Ushindi wa mabao mawili kwa bila iliopata timu ya taifa ya Uhispania
dhidi ya Honduras katika Fainali za Kombe la Dunia zinazoendelea nchini
Afrika Kusini, umeipa matumaini timu ya Uhipania, ya kusonga mbele
katika mashindano hayo.
Ushindi huo wa Uhispania ulikuja baada ya timu ya taifa ya Ureno kuinyeshea mvua ya magoli timu ya taifa ya Korea Kaskazini jioni ya jana Jumatatu.
Timu ya Ureno iliichabanga bila huruma Korea Kaskazini kwa kuichapa mabao 7-0, na hivyo nayo kupata matumaini ya kuingia katika mzunguko wa ili wa michuano hiyo.
Katika mechi nyingine iliyochezwa jana, timu ya Taifa ya Chile ilihakikisha inakuwa karibu mno kusonga mbele na kuingia katika mzunguko wa pili wa 16 bora baada ya kuishinda Uswisi bao moja kwa bila.
Leo Jumanne tarehe 22 Juni, mechi nne zitachezwa katika viwanja tofauti, mbili-mbili kwa wakati mmoja. Afrika Kusini itamenyana na Ufaransa na wakati huo huo Mexico itakuwa inapimana misuli na Uruguay zote za kundi A.
Timu nyingine za kundi B zitapambana baada ya mechi hizo za kundi A. Wakati Nigeria itakapokuwa inapimana nguvu na Korea Kusini katika uwanja wa Moses Mabhida, timu nyingine za kundi B za Ugiriki na Argentina zitakuwa zinamenyana wakati huo huo kwenye uwanja wa Peter Mokaba.

Hatima ya Bafana Bafana na Ufaransa leo katika Kombe la Dunia
Mexico na Uruguay /Nigeria na
K.Kusini / Argentina na Ugiriki.
Siboniso Gaxa ,mlinzi wa Bafana bafana (2) atazima hujuma za
wafaransa leo ?Baada ya Spain, mabingwa wa ulaya jana usiku ikitamba na David Villa, kuipiga kumbo Hondurus kwa mabao 2:0,macho ya mashabiki hasa wa nyumbani Afrika Kusini , yanakodolewa mpambano wa alaasiri ya leo kati ya wenyeji-Bafana Bafana na Ufaransa-timu ambayo inaonekana kusambaaratika .Mpambano wapili ambao pia utaamua hatima ya Afrika Kusini na Ufaransa, ni ule unaochezwa sambamba kati ya Mexico na Uruguay.
Timu hizi mbili za Amerika ya kati na kusini, zinahitaji kutoka sare tu, ili kila moja ikate tiketi yake kwa duru ya pili.Kufanya hivyo, lakini , kunakumbusha kashfa ya Kombe la Dunia,1982 huko Spain, pale Ujerumani na Austria,zilipopanga matokeo na kuitoa mhanga Algeria.
Swali linaloulizwa na mashabiki wa Afrika Kusini na Afrika nzima, ni
Je: Leo mazumari ya "vuvuzela" yatahanikiza kwa mara ya mwisho au
la.Afrika Kusini, lazima iishinde Ufaransa na kutumai Mexico na Uruguay,
zinafungana. Ama sihivyo, Kombe la Dunia 2010 ,la kwanza barani Afrika,
litamalizika kabla ya wakati na sio tu kwa Bafana Bafana, bali hata kwa
Ghana,yenye miadi kesho na Ujerumani katika mpambano wa kufa-kupona kwa
kila moja.
PARREIRA ANA TURUFU GANI ?
Kocha wa Bafana bafana,mbrazil Carlos Parreira,ameahidi kufanya
mabadiliko 5 katika kikosi kilichozabwa mabao 3-0 na mabingwa wa kwanza
kabisa wa dunia-Uruguay.
Kumekuwapo pia mfarakano katika kikosi hicho cha Bafana
Bafana.Wachezaji wa mkoa wa Kwazulu-Natal, yasemekana hawakufurahishwa
na kutocheza kwa ari kwa wenzao kutoka klaubu za Johannesberg na
Pretoria. Hatahivyo, mazumari ya mashabiki wa Bafana bafana, yatazamiwa
kuhanikiza leo alao kwa mara ya mwisho. Kocha Parreira amesma kwamba,
wanawaheeshimu wafaransa lakini, hawawaogopi.Ufaransa, iliilaza Afrika
kusini 3:0 katika Kombe la Dunia, 1998 huko Ufaransa.
UFARANSA NA HATIMA YAKE ?
Ufaransa,makamo bingwa wa dunia 2006 na mabingwa nyumbani, 1998
waliaibishwa na walipochapwa mabao 2:0 na Mexico.Hii ilitanguliwa na
sare ya 0:0 na Uruguay. Kocha wa kutatanisha wa Ufaransa, Raymond
Domenech, ameungama aliposema, " Sasa, tunnahitaji miujiza kusonga
mbele."
Kampeni ya makamo-bingwa hawa wa dunia, ilikumbwa na msukosuko baada
ya wachezaji wa kikosi cha Les B lue,walipogoma kufanya mazowezi ili
kulalamika kwa kutimuliwa mwenzao ,mshambulizi wa Chelsea, Nicolas
Anelka.
Cha kuangalia leo pia, mbali na mpambano kati ya Ufaransa na Afrika
kusini mjini Bloemfontein, ni vipi Uruguay na Mexico, zitakavyocheza.Je,
zitatoka sare huko Rustenburg ? Itakua kashfa nyengine ? Moja ni
wazi,ili wasonge mbele, tangu wafaransa hata Bafana bafana, watapaswa
kuigiza Ureno ilivyocheza jana na kutia mabao mengi.
Leo usiku, itakua zamu ya Nigeria kucheza mpambano wake wa mwisho na
Korea ya Kusini, kabla kuwafuata Simba wa nyika
Kameroun,nyumbani.Nigeria, haina pointi wakati Korea ya kusini, ina
pointi 3. Sambamba na mpambano huo, Argentina, inayopigiwa upatu kuvaa
tena taji la dunia kama Brazil,inamaliza duru hii na Ugiriki.
Mwandishi : Ramadhan Ali
0 comments:
Post a Comment