Mahojiano na mgombea urais Zanzibar Dr.Gharib Bilal
Mji Mkongwe wa Zanzibar
Kinyanganyiro cha kumtafuta atakayekuwa mgombea wa kiti cha Urais kwa niaba ya chama tawala CCM nchini Tanzania kimeanza.
Mji Mkongwe wa Zanzibar
Wakati kwa upande wa Jamhuri ya Muungano ni Rais wa sasa Jakaya Kikwete, shauku kubwa zaidi ni huko Zanzibar ambako rais wa sasa Amani Karume anamaliza muda wake baada ya mihula miwili kwa mujibu wa katiba.
Tayari wanasiasa wanane wameshachukua fomu akiwemo Makamu wa rais wa Tanzania Dr.Ali Mohamed Shein na aliyekuwa Waziri kiongozi wa Zanzibar Dr.Gharib Bilal ambaye hii ni mara yake ya tatu kuwania kiti hicho, baada ya kufanya hivyo mwaka 2000 na mwaka 2005 kabla ya kutakiwa na viongozi wa ngazi ya juu wa CCM kuondoa jina lake.
Mohamed Abdul-Rahman amezungumza punde na Dr. Bilal na kwanza anaelezea kwanini akaamua kuchukua fomu na kugombea tena safari hii?
Interview :Mohamed Abdul-Rahman/Dr Gharib Bilal.
Maafisa watatu wa kulinda amani wa UNAMID wauawa Darfur
Maafisa watatu
wa kulinda amani wameuliwa kwa kupigwa risasi na watu wenye silaha huko
Darfur, magharibi mwa Sudan.
Maafisa hao wameuawa wakati walipokuwa
wanalinda amani katika kambi moja kwenye eneo la Nertiti la Darfur
Magharibi.
Kemal Saiki, mkurugenzi wa masuala ya mawasiliano wa
kikosi cha kulinda amani ya Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa UNAMID
amenukuliwa akisema kwamba, karibu watu 20 wenye silaha walivamia eneo
hilo na kuua maafisa watatu wa kulinda amani wa kikosi hicho kwa kutumia
silaha za otomatiki.
Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa, watu
wapatao laki tatu wameshauawa na wengine milioni 2.7 wameyakimbia
makazi yao tangu jimbo la Darfur lilipoanza kukumbwa na machafuko mwaka
2003
0 comments:
Post a Comment