Mshukiwa wa shambulizi akiri makosa Marekani
Mtu anayedaiwa kupanga
njama ya kulipua bomu lililotegwa ndani ya gari katika bustani la Times
Square mjini New York Marekani, mwezi May, amekiri mashtaka yote kumi
dhidi yake.
Faisal Shahzad raia wa Pakistan, amekiri
kumiliki zana zenye maangamizi makubwa akiwa na nia ya kutumia katika
njama yake iliyotibuka.
Shahzad aliyekamatwa siku mbili baada ya
shambulizi hilo wakati akijaribu kuondoka nchini humo kuelekea Dubai,
alikiri kugeza gari lake lililokuwa na bomu karibu na eneo la Times
Square jumamosi jioni.
Bomu hilo lilipatikana baadaye huku stakabadhi
za mahakamani zikidai kuwa bwan Shazhad alipokea pesa pamoja na mafunzo
kuhusu namna ya kulipua mabomu kutoka kwa kundi la Taleban nchini
Pakistan.
Hata hivyo alisema yuko tayari kukiri makosa
hayo kuonyesha kuwa Marekani ingali inakabiliwa na tisho la mashambulizi
zaidi ikiwa hawatondoka nchini Afghanistan na Iraq.
Ajali ya ndege msituni Congo
Maafisa wakuu nchini
Congo wamethibitisha kutokuwepo manusura wa ajali ya ndege iliyotokea
kati ya msitu wa Congo Brazaville na Cameroun siku ya Jumanmosi.
Ndege hiyo ilikuwa imewabeba wakurugenzi ya
makampuni ya madini wengi wakiwa raia wa Australia.
Watu hao akiwemo mfanyabishara na tajiri mkubwa
nchini Australia, Ken Talbot walikuwa safarini kutoka Cameroun kuzuru
mgodi wa chuma, nchini Congo.
Takriban Maiti wote walipataikana, ingawa waziri
wa mambo ya nje wa Australia,itachukua muda kabla ya kuwatambua na
kisha kuwarejesha nyumbani maiti.
Kiini cha ajali kingali kujulikana.
bbc swahili
bbc swahili
0 comments:
Post a Comment