Maafisa nchini Kyrgystan
wametangaza hali ya hatari nchini humo na kuweka marufuku ya kutoka nje
katika mji wa pili wa Osh pamoja na miji mingine iliyoko karibu,
kufuatia mapigano yaliyozuka na kusababisha vifo vya watu kumi na saba
na kuwajeruhi wengine wengi .
Kwa mujibu wa serikali, vurugu ilizuka kati ya
makundi mawili ya vijana wa mtaa na kukithiri kuwa mapigano ya
kufyatuliana risasi usiku kucha.
Osh ni mji wa kusini mwa nchi hiyo, na eneo la
watu wa kabila la Uzbek, linaloaminika kuwa ngome kuu ya aliyekuwa rais
Kurmanbek Bakiyev aliyeng'olewa mamlakani mwezi Aprili.
Tangu mapinduzi hayo, serikali ya mpito imekuwa
na wakati mgumu kudhibiti usalama na sasa kuna wasiwasi wa kuzuka
mapigano kati ya makabila ya Kyrgyz na Uzbek.
BBC SWAHILI
BBC SWAHILI
0 comments:
Post a Comment