Kiongozi wa Upinzani nchini Burundi Agathon Rwasa ametoweka na
inaaminika kuwa amekimbilia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Rwasa ambaye anaongoza chama cha FNL anaituhumu serikali kuwa imehusika na wizi wa kura katika mkondo wa uchaguzi unaoendelea nchini humo. Rwasa ni kiongozi wa zamani wa waasi na aliweka silaha chini mwaka jana kufuatia mchakato wa amani uliomaliza mgogoro wa miaka 13 katika nchi hiyo ya eneo la Afrika ya Kati.
Duru za usalama nchini Burundi zinasema Rwasa alionekana akitoka katika nyumba yake iliyoko mtaa wa Kiriri mjini Bujumbura mapema Jumatano alfajiri. Imearifiwa kuwa aliingia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa msaada wa wanamgambo wa Mai-Mai. Burundi ilitumbukia tena katika mgogoro wa kisiasa baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa wa Mei ambapo wapinzani wanakilaumu chama tawala cha Rais Pierre Nkurunziza kuwa kilihusika na wizi wa kura. Rwasa alionekana kama mpinzani mkuu wa rais Nkurunziza katika uchaguzi wa rais wa Juni 28 lakini yeye na wagombea wote wa upinzani wamejiondoa katika kinyang'anyiro hicho na hivyo kumuacha rais wa sasa kuwa mgombea pekee.
Akihojiwa na televisheni ya al Jazeera ya nchini Qatar, Khalil Ibrahim, kiongozi wa kundi hilo la JEM amedai kuwa amani haiwezi kupatikana Darfur bila ya kushirikishwa kundi lake.
Baada ya waasi hao wa JEM kukataa kuendelea na mazungumzo ya amani kwa upatanishi wa Qatar, serikali ya Sudan imeamua kuendeleza mazungumzo hayo na kundi LJM mjini Doha mazungumzo ambayo yamelifanya kundi la waasi wa JEM litoe radiamali likidai kuwa yatafeli.
Rwasa ambaye anaongoza chama cha FNL anaituhumu serikali kuwa imehusika na wizi wa kura katika mkondo wa uchaguzi unaoendelea nchini humo. Rwasa ni kiongozi wa zamani wa waasi na aliweka silaha chini mwaka jana kufuatia mchakato wa amani uliomaliza mgogoro wa miaka 13 katika nchi hiyo ya eneo la Afrika ya Kati.
Duru za usalama nchini Burundi zinasema Rwasa alionekana akitoka katika nyumba yake iliyoko mtaa wa Kiriri mjini Bujumbura mapema Jumatano alfajiri. Imearifiwa kuwa aliingia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa msaada wa wanamgambo wa Mai-Mai. Burundi ilitumbukia tena katika mgogoro wa kisiasa baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa wa Mei ambapo wapinzani wanakilaumu chama tawala cha Rais Pierre Nkurunziza kuwa kilihusika na wizi wa kura. Rwasa alionekana kama mpinzani mkuu wa rais Nkurunziza katika uchaguzi wa rais wa Juni 28 lakini yeye na wagombea wote wa upinzani wamejiondoa katika kinyang'anyiro hicho na hivyo kumuacha rais wa sasa kuwa mgombea pekee.
Kiongozi wa waasi wa JEM la Darfur adai kuwa mazungumzo ya Doha yatafeli
Huku serikali ya Sudan ikiendelea na juhudi zake za
kuleta amani katika maeneo yote ya nchi hiyo, kundi moja la waasi wa
Darfur ambalo limekataa kushiriki katika mazungumzo ya amani ya Doha,
limedai kuwa, mazungumzo hayo yatafeli.Akihojiwa na televisheni ya al Jazeera ya nchini Qatar, Khalil Ibrahim, kiongozi wa kundi hilo la JEM amedai kuwa amani haiwezi kupatikana Darfur bila ya kushirikishwa kundi lake.
Baada ya waasi hao wa JEM kukataa kuendelea na mazungumzo ya amani kwa upatanishi wa Qatar, serikali ya Sudan imeamua kuendeleza mazungumzo hayo na kundi LJM mjini Doha mazungumzo ambayo yamelifanya kundi la waasi wa JEM litoe radiamali likidai kuwa yatafeli.
kiswahili radio
0 comments:
Post a Comment