Obama amfuta kazi generali McChrystal
Rais wa Marekani, Barack
Obama, amemteua mmoja wa maafisa wake wakuu jeshini Generali David
Petraeus, kama kamanda mkuu wa majeshi yote ya kigeni nchini
Afghanistan.
Hii ni kufuatia kuachishwa kazi ghafla kwa
,Generali Stanley McChrystal kuhusu matamshi yake ya kuhujumu serikali
ya Obama.
Kulingana na rais Obama matamshi ya McChristal
yameonyesha hana imani na serikali na pia ni ya kuhujumu jeshi
analolihudumia.
Jenerali McChrystal aliitwa kutoka Afghanistan
kwenda Washington kujieleza kutokana na kauli aliyoitoa dhidi ya
utawala wa Marekani.
Matamshi aliyotatoa bwana McChrystal
yamechapishwa kwenye jarida la Rolling Stone.
Mwandishi wa BBC wa maswala ya usalama alisema
kuwa generali Petraeus alikuwa miongoni mwa watu waliopelekwa vitani
Iraq na kubuni sera ambazo sasa zinatumika kutafuta usalama na kumaliza
vita nchini humo.
**************************
Polisi nchini Afrika
Kusini wameachilia washukiwa wawili waliokamatwa kufuatia jaribio la
kumuua kamanda wa zamani wa jeshi la Rwanda mjini Johannesburg
Kayumba Nyamwasa.
Kwa mujibu wa msemaji wa polisi washukiwa
wengine wanne waliosalia watafikishwa mahakamani tarehe ishirini na tisa
mwezi ujao.
Luteni Generali Kayumba Nyamwasa alikuwa
anarejea nyumbani Jumamosi iliyopita wakati alipopigwa risasi tumboni na
mtu asiyejulikana.
Bwana Nyamwasa angali anapata nafuu. Mkewe
amedai serikali ya Rwanda inahusika na njama ya kumuua generali huyo wa
zamani, madai ambayo Rwanda imekanusha.
0 comments:
Post a Comment