Bastian Schweinsteiger(kushoto) na Lukas Podolski(kulia) wa
Ujerumani, wakikwaruzana na Kwadao Asamoah wa Ghana (kulia) katika
mchuano wa Kombe la Dunia uwanjani Soccer City, Johannesburg.
Wayne Rooney wa Uingereza(katikati) akikumbana na Aleksander
Radosavljevic na Miso Brecko(kulia) wa Slovenia katika mchuano wa Kombe
la Dunia
Ujerumani imesonga mbele katika duru
ya pili ya michuano ya kuwania Kombe la Dunia inayoendelea nchini
Afrika Kusini.
Hiyo jana, Ujerumani ilinusurika, baada ya kuilaza
Ghana kwa bao 1-0 katika mchezo wa kufa kupona, pande hizo mbili
zilipokumbana uwanjani Soccer City mjini Johannesburg.
Baada ya kuchuana kwa dakika sitini nzima, Mesut
Oezil wa Ujerumani, aliuvurumisha mpira katika wavu wa Ghana na hivyo
kuinusuru Ujerumani kufunga virago na kurejea nyumbani katika duru ya
mwanzo ya Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza kabisa.
Hata hivyo, Ghana iliitoa jasho Ujerumani na
imethibitisha kuwa wao kweli ni nyota. Ghana ni timu pekee kutoka Afrika
kubaki katika kundi la timu 16 za mwisho, katika kinyanganyiro hicho
cha Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini. Nyota hao wa Ghana, watakumbana
na Marekani jumamosi ijayo. Hiyo jana Marekani iliifunga Algeria bao
1-0 na Australia nayo iliicharaza Serbia mabao 2-1.Uingereza pia hiiyo jana ilinusurika kufunga
virago, baada ya kuikandika Slovenia bao 1-0.
Uingereza itateremka tena uwanjani siku ya Jumapili
kwa mchezo unaongojewa kwa hamu kubwa. Siku hiyo, Uingereza itakwaruzana
na Ujerumani.
Bendera ya Palestina yapeperushwa hewani mechi ya Algeria na MarekaniUwanja wa Loftus Versfeld huko Tshwane mjini Pretoria jana ulishuhudia kupeperushwa bendera ya Palestina wakati Bill Clinton, Rais wa zamani wa Marekani alipokuwa katika uwanja huo kushuhudia mechi kati ya nchi yake na Algeria.
Bendera hiyo Palestina ilikuwa kivutio kikubwa kwa waandishi wa habari, wapiga picha na mashabiki waliokuwepo uwanjani hapo hususan kutokana na kuwa si timu ya Palestina iliyokuwa inacheza na Marekani.
Shabiki mwingine alikuwa amejiandika Allahu Akbar na Ghaza Madhlumu na kulikuwa pia na maandishi ya Lan Nansaaka Ghaza yaani kamwe hatuwezi kukusahau Ghaza, yote hayo yakionyesha uungaji mkono wao kwa wananchi wanaodhulumiwa wa Palestina.
Ingawa mechi hiyo
ilikuwa ni kati ya Marekani na Algeria ambayo ni nchi za Kiarabu na
Kiislamu lakini kitendo hicho cha mashabiki kilitoa ujumbe maalumu kwa
Wamarekani huku maafisa usalama apolisi waliokuwepo kwenye uwanja huo
wakiwaacha mashabiki hao bila ya kuwafanya chochote.
Marekani
inaziunga mkono kibubusa jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel huku
wananchi wa Ghaza wakiendelea kuteseka kutokana na jinai hizo za
Wazayuni
ENG-Jermain
DEFOE
Katika mtanange huo Mchezaji Jermain
DEFOE wa England alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo kati ya England na Slovenia.
USA-Landon
DONOVAN
Katika mtanange huo Mchezaji Landon
DONOVAN wa USA alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo kati ya USA
na Algeria
GER-Mesut
OEZIL
Katika mtanange huo Mchezaji Mesut
OEZIL wa Germany alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo kati ya Germany
na Ghana.
AUS-Tim
CAHILL
Katika mtanange huo Mchezaji Tim
CAHILL wa Australia alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo kati ya Australia
na Serbia.
0 comments:
Post a Comment