Kamanda wa jeshi la Marekani Afghanistan kutiwa kiti moto leo mbele ya Obama |
Kamanda wa jeshi la Marekani na vikosi vya majeshi ya NATO nchini
Afghanistan Jenerali Stanley McChrystal anatazamiwa kusailiwa leo na
Rais wa nchi hiyo Barack Obama baada ya kuwashambulia na kuwachezea
shere viongozi wa ngazi za juu wa serikali ya Washington akiwataja kuwa
ni dhaifu na wasiojali. Matamshi hayo yamezusha mivutano baina ya
makamanda wa jeshi la Marekani na wanasiasa wa nchi hiyo katika kipindi
hiki kigumu ambapo askari wa kigeni wanakabiliwa na hali ngumu huko
Afghanistan.
Jenerali Stanly McChrystal ambaye alikuwa kihojiwa na jarida la Rolling Stone amekebehi Rais Obama na wasaidizi wake hususan makamu wa Rais Joe Biden. Msemaji wa Ikulu ya Marekani ameashiria kwamba kuna uwezekano jenerali huyo akauzuliwa licha ya kuomba msamaha kuhusu matamshi yake. Katika moja ya mashambulizi yake dhidia ya viongozi wa kisiasa wa serikali ya Obama, Jenerali McChrystal amemtaja Biden kuwa ni mng'ataji na balozi wa nchi hiyo huko Afghanistan kuwa ni "msaliti."
*******************
Mbeki: Wapalestina ndio watakaochagua wenyewe njia na mbinu za kupambana na Wazayuni
Jenerali Stanley McCrystal atakutana ana kwa ana na rais Obama
kuhusu matamshi yake.
Rais Barack Obama wa Marekani amesema matamshi
yaliyotolewa na Jenerali Stanley McChrystal yanaonesha kwamba ametoa
hukumu isiyokuwa sahihi na kwamba angali anachunguza majibu ya matamshi
hayo. Jenerali Stanly McChrystal ambaye alikuwa kihojiwa na jarida la Rolling Stone amekebehi Rais Obama na wasaidizi wake hususan makamu wa Rais Joe Biden. Msemaji wa Ikulu ya Marekani ameashiria kwamba kuna uwezekano jenerali huyo akauzuliwa licha ya kuomba msamaha kuhusu matamshi yake. Katika moja ya mashambulizi yake dhidia ya viongozi wa kisiasa wa serikali ya Obama, Jenerali McChrystal amemtaja Biden kuwa ni mng'ataji na balozi wa nchi hiyo huko Afghanistan kuwa ni "msaliti."
*******************
Mbeki: Wapalestina ndio watakaochagua wenyewe njia na mbinu za kupambana na Wazayuni
Rais wa zamani wa Afrika Kusini Thambo Mbeki amesema kuwa wananchi wa Palestina hawawezi kupata haki zao zilizoghusubiwa ila kwa kupitia njia ya mapambano ambayo wao wenyewe ndio wenye haki ya kuchagua njia na mbinu zake. Thabo Mbeki amesema kuwa mazungumzo ya muda mrefu kati ya Wapalestina na utawala haramu wa Israel hayajazaa matunda yotote hadi hivi sasa. Amesisitiza kuwa ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Palestina ni kielelezo kwamba hali ya mambo bado haijaboreka wala hakuna maendeleo yoyote.
Rais wa zamani wa Afrika Kusini amewataka wapatanishi wa kimataifa kutafuta mbinu za kutatua mgogoro wa Palestina na akasisitiza kuwa nchi yake inatetea haki za wananchi wanaokandamizwa wa Palestina.
******************
Mapigano makali yanaendelea Darfur, mazungumzo kuanza tena leo Doha
Mapigano makali kati ya jeshi la serikali ya Sudan na wapiganaji wa Harakati ya Uadilifu na Usawa JEM yameendelea kuripotiwa katika jimbo la Darfur huko magharibi mwa Sudan huku kila upand ukidai kupata ushindi. Jeshi la Sudan limetangaza kuwa limeua waasi 43 na kujeruhi wengine 90 katika mapigano yaliyotoklea kwenye eneo la Uzban na kwamba askari wake 7 wameuawa na 11 kijeruhiwa.
Harakati ya uadilifu na Usawa imekiri kutokea mapigano hayo lakini imedai kuwa imepata ushindi licha ya kwamba haikutoa takwimu zozote. Kiongozi mmoja wa harakati ya JEM amekiri kwamba kamanda mmoja wa ngazi za juu ameuawa katika mapigano hayo na kwamba wenzake watatu wamejeruhiwa.
Hadi sasa jeshi la kulinda amani la Umoja wa Afrika halijatoa maelezo yoyote kuhusu mapigano hayo ingawa limesisitiza kuwa raia wa kawaida wameathiriwa.
Mapigano hayo yametokea huku wawakilishi wa serikali ya Khartoum wakitarajiwa kuanza duru nyingine ya mazungumzo ya amani na muungano wa makundi ya waasi wa Darfur hii leo mjini Doha, Qatar.
kiswahili radio
0 comments:
Post a Comment