SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, June 23, 2010

Afrika kusini, Ufaransa wafunga virago,Argentina, Korea Kusini kuiona hatua ya mtoano


Afrika Kusini imefanikiwa kutoka kifua mbele dhidi ya Ufaransa kwa kuinyuka mabao 2-1, lakini licha ya ushindi huo Afrika Kusini imekuwa timu ya kwanza mwenyeji kutolewa katika raundi ya kwanza kwenye michuano ya kombe la dunia, nao ufaransa wanaoshika mkia kwenye kundi A kwa kuwa na pointi moja pia wameyaaga mashindano hayo.
Uruguay imemaliza katika raundi ya kwanza ikiwa kileleni kwenye kundi A kwa kuwa na pointi 7 baada ya kuwararua Mexico kwa goli 1-0, ingawa mexico imeshindwa katika mchezo huo bado imepata nafasi ya kuingia katika raundi ya mtoano.
Kocha wa Nigeria amehuzunishwa sana kwa timu yake kutolewa nje ya michuano ya kombe la dunia inayoendelea huko Afrika Kusini, super Eagles wametoka sare ya 2-2 katika mechi iliyochezwa tarehe 22 dhidi ya korea kusini, matokeo hayo yameisafishia njia korea kusini kuingia kwenye raundi ya pili.
Argentina ambao wanaongoza katika kundi B, tayari walishaingia kwenye hatua ya pili kutokana na kufanya vizuri katika mechi mbili za mwanzo, na katika mechi ya tarehe 22 iliweza kuibanjua Ugiriki kwa magoli 2 kwa nunge, jambo ambalo limeifanya ugiriki iage mashindano hayo.

0 comments:

Post a Comment