SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, June 21, 2010

Kaimu Rais Goodluck kimya kuhusu uchaguzi

Rais Goodluck Jonathan
    Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan amakataa kuzungumzia ikiwa atawania kiti cha urais, katika uchaguzi mkuu nchini humo mwaka ujao.
   AKihutubia taifa kupitia kwa televisheni ya kitaifa, Jonathan ameliambia taifa kuwa anasubiri wakati muafaka ili kutangaza uamuzi wake.
   Waandishi wa habari wanasema uamuzi wake wa kuwania kiti cha urais, utazua mjadala mkali, kwa sababu anatoka eneo la kusini ambako idadi kubwa ya raia ni waumini wa dini ya Kikristu.
   Kwa mujibu wa mkataba ambao haujanakiliwa, popote na chama tawala nchini humo, rais atakaye chaguliwa anapaswa kutoka eneo la Kaskini ambako idadi kubwa ya raia ni Waislamu.
   Jonathan alitwaa madaraka ya kuliongoza Nigeria baada ya kifo cha mtangulizi wake, UmaruYar'Adua, ambaye alitoka k eneo la Kaskazini na alitarajiwa kuwania muhula mwingine kama rais.  

Niger yakabiliwa na tisho la Njaa
Ramani ya Niger
    Mashirika mawili makuu ya misaada yamezindua ombi la dharura kusaidia mamilioni ya watu nchini Niger wanaokumbwa na baa la njaa.
   Mashirika hayo Save the Children na Oxfam, yanasema kuwa hali sio mbaya sana kwa sasa ingawa ingawa yanataka kuzuia haliiliyotokea miaka mitano iliyopita ambapo watu milioni tatu unusu waliathirika kutokana na ukosefu wa chakula.
Wengi pia walikumbwa na utapiamlo wakati huo.
   Waziri wa elimu ya juu wa nchi hiyo amsema serikali imeweza kudhibiti hali ingawa hana uhakika kwamba watu hawaathrika kutokana na njaa hiyo.
BBC SWAHILI

0 comments:

Post a Comment