SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, June 21, 2010

JK KUCHUKUA FOMU ZA KUGOMBEA URAIS LEO



MWENYEKITI WA CCM NA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DK. JAKAYA MRISHO KIKWETE LEO ANAPIGA RASMI KIPYENGA CHA CHAMA HICHO TAWALA CHA MBIO ZA UCHAGUZI MKUU WA RAIS NA WABUNGE KWA KUCHUKUA FOMU ZA KUGOMBEA KATIKA MAKAO MAKUU YA CCM MJINI DODOMA AMBAKO SHAMRASHAMRA YA TUKIO HILO LIMEANZA MAPEMA ASUBUHI HII.

Shamrashamra za JK kuchukua fomu za kugombeaUrais

JK akipokea fomu za kugombea urais toka kwa katibu
mkuu wa CCM Mh. Yusuf Makamba mchana huu dodoma
"....Kila la kheri ..." anaonekana Mh. Yusuf Makamba
akimwambia JK baada ya kumkabidhi fomu za kugombea Urais

JK akionesha fomu kwa umati mkubwa wa wana CCM
Waliojitokeza kushuhudia hafla hii Mama Salma na watoto walikuwepo kushuhudia Mama Salma Kikwete na Mama Pinda katika hafla hii Vijana wa UVCCM wakihakikia kadi za wanachama wanaomdhamini JK Uhakiki wa wadhamini wa JK waendelea Wengi wajitokeza kumdhamini JK Uhakiki wa wadhamini wa JK unafanyika kwa makini Foleni ya wana CCM wanaotaka kumdhamini JK

JK mgeni rasmi miaka 100 ya KKKT Bukoba
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Magharibi Mhashamu Elisa Buberwa akimkaribisha Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika viwanja vya kanisa la Kashura mjini Bukoba Jumapili kushiriki katika maadhimisho ya jubilii ya miaka mia moja tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo. Katikati ni Mkuu wa Kanisa la KKKT nchini Askofu Dr.Alex Malasusa. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Mkuu wa kanisa la KKKT nchini Tanzania Askofu Dk. Alex Malasusa wakati wa maadhimisho ya jubilei ya miaka 100 tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo iliyofanyika katika kanisa la KKKT la Kashura, wilayani Bukoba. mkoa wa Kagera.Baadhi ya waumini wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Magharibi wakihudhuria sherehe za kuadhimisha miaka mia moja tangu kuanzishwa kwa kanisa hili huko Kashura Bukoba mjini Jumapili mchana.

0 comments:

Post a Comment