SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Sunday, June 20, 2010

MH. RAIS JK ZIARANI RUKWA
Mama wa Waziri mkuu Alberina Kasanga akimzawadia kuku JK alipowatemebelea nyumbani kwao eneo la Kibaoni,wilayani Mpanda,mkoa wa rukwa jana mchana. Kulia ni Mzee Xaveri Kayanza Pinda,Baba ya Waziri mkuu mizengo Pinda
Akiwa pamoja na wazazi wa Waziri Mkuu mhehimiwa mizengo Pinda huko nyumabni kwao Kibaoni, wilayani Mpanda,mkoa wa Rukwa jana mchana.Kushoto ni Mzee Xaveri Kayanza Pinda(80) Baba wa Waziri Mkuu na kulia ni Mama Albertina Kasanga(70) Mama wa Waziri Mkuu
Mtaalamu wa Maabara katika hospitali ya mkoa wa Rukwa bwana Dodea Mlenda akimpa maelezo Rais Jakaya Mrisho Kikwete jinsi mashine mpya za kisasa za uchunguzi wa maradhi zinavyofanya kazi muda mfupi baada ya Rais Kuzindua maabara ya kisasa katika hospitali ya mkoa wa Rukwa jana asubuhi.Maabara hiyo ya hospitali ya mkoa wa Rukwa ni kati ya maabara 23 zinazojengwa katika mikoa mbalimbali nchini kwa msaada wa shirika la Abbott Fund lenye makao yake nchini Marekani.Kushoto ni Mbunge wa Kwela Chrisant Mzindakaya na watatu kutoka kushoto ni Mwakilishi wa Waziri wa Afya Dr.Pamela Sawa.JK akikata utepe kuzindua ujenzi wa mitambo mipya ya kuzalisha umeme mjini Sumbawanga jana asubuhi.Mitambo hiyo itauwezesha mji wa Sumbawanga na wilaya za jirani kupata umeme wa uhakika.Watatu kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja,wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO mhandisi Willoima Mhando na wane kushoto ni meneja mahusiano wa TANESCO Badra Masoud. 
michuzi blog

0 comments:

Post a Comment