Waziri mkuu wa Usrael Benjamin Netanyahu anaweza pia kuitwa na
jopo kutoa ushahidi wake juu ya shambulio dhidi ya meli za misaada
zilizokuwa zikielekea Gaza.
Israel inaweza kuongeza jukumu la
uchunguzi wake juu ya shambulio lililofanywa dhidi ya meli zilizokuwa
zikipeleka misaada katika ukanda wa Gaza, kwa kuruhusu jopo lililoundwa
kuchunguza kisa hicho kuwahoji mashahidi.
Taarifa iliyotolewa na serikali ya Israel, imesema kiongozi wa jopo
hilo la uchunguzi Jaji Jacob Turkel amewasilisha ombi kupanuliwa
kwa uchunguzi huo kwa kuwawezesha mashahidi kutoa ushahidi wao
baada ya kula kiapo.
Jopo hilo linaloongozwa na Jacob Turkel, Jaji mstaafu wa mahakama
kuu ya Israel, lilianza uchunguzi wake siku ya Jumatatu na kwamba
Waziri mkuu wa nchi hiyo Benjamin Netanyahu na waziri wake wa
ulinzi wanaweza pia kuitwa kutoa ushahidi wao kuhusiana na tukio
hilo lililotokea Mei 31, ambapo raia tisa wa Uturuki waliuawa.
Kiongozi huyo wa jopo, amesema juukumu lao ni kuchunguza kama
kuzingira kulikofanywa na jeshi la majini la Israel na msafara wa meli
za misaada uliendana na sheria za kimataifa na pia uchunguzi ya
kitendo cha waratibu wa msafara wa meli na washiriki wake.
Miongomi mwa wanaounda jopo hilo ni pamoja na mtaalamu wa
Israel wa masuala ya sheria za kimataifa, mkuu wa zamani wa jeshi,
pamoja na waangalizi wawili wa kigeni, ambao ni mshindi wa tuzo ya
Nobel na mwanasheria wa Canada Ken Watkin, pamoja na David
Trimble, mwanasiasa kutoka Ireland ya kaskazini, ambaye alisema
kuwa wote wamejidhatiti kuona uchunguzi unakuwa wa kuwajibika na
kutumai kuwa utaweza hatimaye kutoa mchango wa maana kwa
amani.
Tukio hilo lilitia doa uhusiano kati ya Israel na Uturuki iliyo nchi
ya
kiislamu ambayo ni mshirika wake muhimu, ambapo toka kutokea
kwa shambulio hilo ili muita nyumbani balozi wake pamoja na kufuta
mazoezi ya pamoja ya kijeshi yaliyokuwa yakifanywa na taifa hilo la
kiyahudi.
Israel iliamua kufanya uchunguzi huo baada ya nchi na jumuia
mbalimbali duniani kulishutumu shambulio hilo, kwa kufikiria kwamba
itapinga pendekezo la Umoja wa Mataifa la kufanyika kwa uchunguzi
wa kimataifa.
Shambulio hilo lililofanya na makomando wa Israel, matokeo yake
liliangazia vizuizi vilivyowekwa na Israel katika ukanda wa Gaza
ambao unadhibitiwa na chama cha Hamas, hali ambayo pia
ilisababisha kulegezwa kwa vizuizi hivyo.
Ikijitetea Israel ilisema kuwa makomando wake ambao walivamia
moja ya meli zilizofadhiliwa na Uturuki kupeleka misaada Gaza,
walikuwa wakitekeleza vizuizi vilivyowekwa kwa ajili ya kuzuia silaha
zisiwafikie wapiganaji wakiislamu walioko katika eneo hilo na
kwamba walifyatua risasi ili kujihami baada ya wanaharakati
waliokuwa ndani ya meli hiyo kuwashambulia visu na marungu.
Mwandishi: Halima Nyanza(Reuters)
0 comments:
Post a Comment