SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, June 25, 2010

Ghadafi na Waziri Mkuu wa Uhispania wajadili mkutano ujao wa Afrika na EU

Sample Image 











Muammar Gaddafi Kiongozi wa Libya amekutana na Jose Luis Rodriguez Zapatero Waziri Mkuu wa Uhispania kujadili ajenda ya mkutano wa Afrika na Umoja wa Ulaya unaoratajiwa kufanyika baadaye mwaka huu. Taarifa zinasema kuwa, viongozi hao wawili wamesisitiza umuhimu wa kutayarishwa vyema duru hiyo ya tatu ya mkutano wa Afrika na Umoja wa Ulaya, ili uchangie kuleta maendeleo barani Afrika na kupunguza wimbi la wahamiaji barani Ulaya. Vilevile Gaddafi na Zapatero wamezungumzia hali ilivyo hivi sasa nchini Iraq na katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.
Uhispania ilikuwa na nafasi kubwa katika kutatua mzozo wa Libya na Uswisi, ambao uliisha mwanzoni mwa mwezi huu baada ya serikali ya Tripoli kumruhusu mfanyabiashara Max Goeldi wa Uswisi iliyokuwa inamshikilia arejee nchini kwao.
**************************
Umoja wa Mataifa wasitisha misaada Darfur kwa sababu za ukosefu wa Usalama 
Sample Image 











Umoja wa Mataifa umesema kwamba ukosefu wa usalama katika eneno la Darfur Magharibi mwa Sudan umepelekea mashirika ya misaada yasimamishe utoaji misaada katika eneo hilo. Taarifa hiyo imetolewa siku mbili baada wafanyakazi wawili wa utoaji misaada raia wa Ujerumani kutekwa nyara na watu wenye silaha katika eneo la Nyala ambako ni makao makuu ya jimbo la Darfur Kusini. Vilevile ikiwa ni siku 3 baada ya kuuawa askari watatu wa kulinda amani wa Rwanda katikati mwa Darfur.
Umoja wa Mataifa pia umeitaka serikali ya Sudan ifanye jitihada za kuwakamata na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria watu ambao wamewashambulia, kuwateka nyara na kuwaibia wafanyakazi wa misaada ya kibinaadamu. Mpango wa Chakula wa Umoja wa mataifa (WFP) umesema kuwa, zaidi ya watu milioni nne wa eneo la Darfur watakosa misaada ya chakula mwezi huu wa Juni, kutokana na sababu mbalimbali zinazokwamisha shughuli za makundi ya utoaji misaada katika eneo hilo.
kiswahili radio

0 comments:

Post a Comment