Ujerumani imefuzu kucheza robo
fainali ya Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini, baada ya kuifunga
England mabao 4-1 katika uwanja wa Free State mjini Bloemfontein.
Mechi hiyo ambayo England walionyesha kulemewa
katika safu ya ulinzi, pia itakumbukwa kwa kukataliwa bao la wazi
lililofungwa katika dakika ya 38 na Frank Lampard.
Ujerumani walitangulia kufunga katika dakika ya 20
kupitia Miroslav Klose, na katika dakika ya 32 Lukas Podolski akaongeza
goli la pili.
Katika dakika ya 37, England walipata kona na
mlinzi Mathew Upson akafunga kwa kichwa kuipatia England goli pekee.
Dakika moja tu baada ya bao hilo Frank Lampard alipiga mpira wa mbali
ambao uligonga juu ya mwamba kabla ya kudunda ndani ya goli la
Ujerumani.
Utata
Lakini mwamuzi Uruguay Jorge Larrionda kutoka
Uruguay alifuata ushauri wa msaidizi wake wa pembeni na kuendeleza
mchezo bila kutambua bao hilo.
Kipindi cha pili kilimalizika Ujerumani wakiongoza
2-1, na majaribio kadhaa ya mashambulizi ya England hayakufanikiwa.
Thomas Mueller alizamisha kabisa matumaini ya
England kwa kufunga mabao mawili katika kipindi cha dakika tatu, moja
katika dakika ya 67 na la nne katika dakika ya 70.
Kocha wa Ujerumani, Joachim Loew, akiwa ameshapata
imani ya ushindi alifanya mabadiliko yaliyoonekana ya kuwapumzisha
washambuliaji muhimu kwa ajili ya robo fainali.
Meneja wa England, Fabio Capello, pia alifanya
mabadiliko kadhaa katika kipindi cha pili kuimarisha ushambuliaji lakini
bila mafanikio.
TAZAMA VIMBWANGA VYA PWEZA ALIYETABIRI USHINDI WA GERMANY DHIDI YA ENGLAND
TAZAMA VIMBWANGA VYA PWEZA ALIYETABIRI USHINDI WA GERMANY DHIDI YA ENGLAND
0 comments:
Post a Comment