Waziri Mkuu wa Uingereza David
Cameron atajadili janga la kumwagika kwa mafuta katika Ghuba ya Mexico
na Rais Barack Obama baadaye hii leo.
Bw Cameron amesema kuwa "ametatizwa na kuwa na
wasiwasi mkubwa" kuhusu athari za kimazingira zilizosababishwa na kisima
cha mafuta cha shirika la BP.
Lakini ofisi ya waziri mkuu ya Downing Street
imesema mazungumzo ya simu na Rais Obama yatakuwa yenye manufaa.
Mhariri wa BBC wa masuala ya kibiashara Robert
Peston alisema shirika la BP linaonekana kuitikia shinikizo za Marekanii
na pia kusitisha malipo ya faida kwa wenye hisa wa shirika hilo.
Wakurugenzi wa shirika hilo watakutana siku ya
Jumatatu kujadili uwezekano wa suala hilo.
Mwandishi wetu alisema " imechukua muda kwa bodi
ya utawala wa BP kufikia uamuzi ikiwa Rais Obama anawataka kusitisha
malipo kwa wenye hisa, na huenda hilo likawa jambo la busara ".
Shirika la BP litasitisha kutoa malipo hayo ya faida yenye thamani ya paundi 1.8bn, hadi hapo litaweza kujua ni kiasi gani cha fedha inatakiwa kulipa kutokana na janga hilo la kumwagika kwa mafuta na kuhakikisha kuwa inaweza kumudu gharama zote zinazohitajika.
Shirika la BP litasitisha kutoa malipo hayo ya faida yenye thamani ya paundi 1.8bn, hadi hapo litaweza kujua ni kiasi gani cha fedha inatakiwa kulipa kutokana na janga hilo la kumwagika kwa mafuta na kuhakikisha kuwa inaweza kumudu gharama zote zinazohitajika.
Mwandishi wetu aliongeza kuwa hata kama gharama
hizo zitapita paundi 20bn, wadadisi wanatarajia kuwa BP inahisi kuwa na
rasilimali za kutosha kumudu gharama hizo.
Mafuta yamekuwa yakimwagika katika Ghuba ya
Mexico tangu mtambo wa kuchimba mafuta chini ya bahari kulipuka tarehe
20 mwezi April katika jimbo la Louisiana, na kuuwa wafanyakazi 11.
Kiasi cha mapipa 40,000 ya mafuta yamekuwa
yakimwagila kila siku hadi tundu lililokuwa linavuja kuzibwa tarehe 3
mwezi June.
Bw Cameron na Chancellor George Osborne
wamekiwshazungumza na Mkuu wa shirika la BP, Carl-Henric Svanberg,
kuhusu janga hilo.
0 comments:
Post a Comment