Timu za taifa za soka za Brazil na Ureno zimeshindwa kutambiana baada ya kutoka sare ya bila kufungana katika mechi ya kundi G, iliyomalizika masaa machache yaliyopita nchini Afrika Kusini. Kwenye mechi hiyo iliyokuwa kali na ya kusisimua, timu hizo mbili ziliridhika kutoka uwanjani bila ya kupatikana mshindi. Kwa matokeo hayo, Brazil na Ureno zitasonga mbele, kwenye mechi za hatua ya mtoano. Kwenye mechi nyingine ya kundi hilo, wawakilishi wa Afrika timu ya taifa ya Ivory Coast yakumbuka shuka wakati kumeshakucha, baada ya kuitandika Korea ya Kaskazini mabao 3-0. Kitimtimu kingine kitashuhudiwa muda mchache ujao, wakati Chile itakapokamuana na Uhispania, na Uswisi itatupa karata yake kwa kupambana na Honduras. Timu za Chile, Uhispania na Uswisi, zote zina nafasi nzuri ya kusonga mbele. Kesho Jumamosi, zitaanza mechi za mtoano, Uruguay ikicheza na Korea ya Kusini na Marekani ikipambana na Ghana.
Friday, June 25, 2010
Brazil na Ureno zapeta, Cote D'voire yakumbuka shuka kumeshapambazuka

Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Friday, June 25, 2010
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
0 comments:
Post a Comment