Jumuiya ya
Afrika Mashariki EAC itatuma timu ya wasimamizi wa uchaguzi wa rais
nchini Burundi unaotarajiwa kufanyika nchini humo siku chache zijazo.
Taarifa ya jumuiya hiyo iliyotolewa mjini Dar es Salaam Tanzania
imeeleza kuwa, kundi hilo la watu 24 litasimamia zoezi la uchaguzi huo
uliopangwa kufanyika tarehe 28 mwezi huu. Hadi hivi sasa kuna hitilafu
kati ya serikali na waasi wa zamani wa Burundi juu ya kugawana madaraka
ya kisiasa na kijeshi, na suala hilo limepelekea kutotelekezwa
kikamilifu makubaliano ya kusitisha mapigano ya mwezi Septemba mwaka
2006. Wiki chache zilizopita ulifanyika uchaguzi wa madiwani, lakini
mrengo wa upinzani ulilalamikia zoezi zima la uchaguzi huo uliokipatia
ushindi chama tawala cha CNDD FDD. Wapinzani nchini Burundi, kwa kauli
moja wametangaza kususia uchaguzi wa rais, na kusababisha kuibuka hali
ya wasiwasi ya kutokea tena mapigano nchini humo.
Friday, June 25, 2010
Nchi za Afrika Mashariki kusimamia uchaguzi wa rais nchini Burundi
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Friday, June 25, 2010
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
0 comments:
Post a Comment