Waziri
wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza
wakati wa uzinduzi wa tamasha la Kimataifa la Filamu la Tanzanite mkoani
Arusha .
Waziri
Nape aliwaambia wadau na waigizaji wa Filamu waliohudhuria uzinduzi wa
Tamasha hilo kuwa hii ni moja ya hatua kubwa kwenye historia ya filamu
nchini na kuahidi Wizara yake itaendelea kutoa ushirikiano mkubwa na
kuhakikisha haki za wasanii hazipotei wala haziliwi na wajanja.
Mkurugenzi
wa Tanzanite One ambao ndio wadhamini wakuu wa Tamasha, Ndugu Faisal
Juma akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Kimataifa la Filamu la
Tanzanite mjini Arusha kwenye hotel ya Mt. Meru
Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akifunua
pazia kuashiria uzinduzi wa Tamasha la kimataifa la filamu la Tanzanite
mjini Arusha.
Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (mwenye
kaunda suti ya kijivu) akiwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Ndugu
Felix Ntibenda kwenye picha ya pamoja na viongozi pamoja na wadhamini
kwenye uzinduzi wa Tamasha la Kimataifa la Filamu la Tanzanite.
Viongozi wa Arusha wakiwa
Baadhi ya watu waliohudhuria uzinduzi huo wa Tamasha la Filamu la Kimataifa la Tanzanite.
Yvonne
Cherry 'Monalisa' pamoja na mama yake, Suzan Lewis 'Natasha' (katikati)
wakifuatilia sherehe uzinduzi wa Tamasha la Filamu la Kimataifa la
Tanzanite kwenye hotel ya Mt. Meru
0 comments:
Post a Comment