Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa
na Michezo Mhe.Nape Nnauye akizungumza na wadau waliopo chiniya wizara
yake pamoja na watumishi wa sekretarieti ya mkoa wa Mara wakati wa ziara
ya kutembelea maeneo yanayohusu sekta za wizara, kupokea taarifa ya
mkoa na kuwapatia vitendea kazi maafisa mawasiliano wa mkoa huo.
Wengine pichani ni Katibu Tawala mkoa wa Mara Bw.Benedict Ole Kuyan(wa
kwanza kulia),Mkuu wa wilaya ya Butiama Bi.Anarose Nyamubi(wa tatu
kulia) na Kaimu meya wa manispaa Bw.Wambura Kajala.
Kaimu Mkuu wa mkoa wa shinyanga
Bi.Josephine Matiro akizungumza jambo wakati wa kumkaribisha Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye baada ya kuwasili
mkoani hapo ili kujua changamoto mbalimbali za watumishi walio chini ya
wizara yake na kuongea na wadau wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo.
Katibu Tawala mkoa wa Mara
Bw.Benedict Ole Kuyan akizungumza na wadau mbali mbali wa sekta za
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo pamoja na watumishi wa serikali wa
mkoa wa Mara leo hii wakati wa Ziara ya Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa
na Michezo Mhe.Nape Nnauye mkoani humo.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa
na Michezo Mhe.Nape Nnauye akipata maelezo kutoka kwa fundi mitambo
mwandamizi wa shirika la utangazaji Tanzania(TBC) Bw.John Igomego jinsi
mitambo yakurushia matangazo ya shirika hilo inavyofanya kazi mkoa wa
Mara.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa
na Michezo Mhe.Nape Nnauye akizungumza na katibu wa chama cha
mapinduzi(CCM) mkoani Shinyanga Alhaj Saad Kusilawe(mwenye kofia ya
njano) kuhusu maendelezo ya uwanja wa kambarage ambao unamilikiwa na
chama hicho mkoani hapo.Mhe.Nape amewaasa viongozi wa mkoa huo kutafta
wadhamini ili kuuboresha uwanja huo.
…………………………………………………………………………………………………………….
Na Daudi Manongi-WHUSM
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa
na Michezo amesema kuwa atahakikisha heshima ya tasnia ya habari
inarudi baada ya kupitishwa kwa mswada wa sheria ya huduma za vyombo
vya Habari.
Waziri Nape ameyasema hayo
alipokuwa katika katika ziara mkoani Mara na Shinyanga na kutembelea
maeneo yanayohusu sekta za wizara hiyo na kupokea taarifa ya mkoa na
kuwapatia vitendea kazi maafisa mawasiliano wa mikoa hiyo.
“Ule mswada utatoa tafsiri ya
mwandishi wa habari,maana mwandishi wa habari lazma awe na sifa.Siku
hizi anaweza kuwa mtu anauza ndizi alafu akajifunza kupiga picha
akajiita na yeye mwandishi wa Habari.Ukifanya ivyo tasnia hii inakosa
heshima,kwaiyo sheria ile itatafsiri nani mwandishi wa habari”Alisema
Nape.
Aidha Waziri Nape alisema kuwa
kwa kufanya hivi sheria hii itatibu tatizo la kulipwa vibaya na wamiliki
wa vyombo vya habari maana mwandishi huyu atakuwa na elimu,maana kama
hana elimu mmiliki ataajili mtu anaejua kusema wa kijuweni alafu ndo
anamuajiri anakuwa mtangazaji wa radio yake kisa tu anajua kusema.
Pamoja na hayo waziri uyo mwenye
dhamana ya wizara nyeti ya habari alisema kuwa sheria hiyo pia
itazungumzia maslahi ya mwandishi wa habari,itawabana wamiliki na mswada
huu ukipita utarudisha heshima ya tasnia hii ya habari katika nchi
yetu.
Akizungumzia upande wa radio
kujenga nchi waziri nape amewaasa waandishi wa habari na watangazaji wa
radio kujenga amani ya nchi yetu kwa kuwaunganisha watanzania kupitia
radio zao na si kuwatenganisha akitolea mfano wa yaliyotokea nchini
Rwanda kwamba radio zilitumika kuhamasisha mauaji.
Mheshimiwa Nape pia amehaidi
kuimarisha vitengo vya mawasiliano serikalini ikiwa ni pamoja na kuwapa
maafisa hao vitendea kazi, pia ameliomba jeshi la polisi kutoa
ushirikiano katika kutoa taarifa na amehaidi kuzungumza na jeshi hilo
ili waandishi hawa waweze kupata taarifa kirahisi.
Waziri uyo yupo katika ziara ya
mikoa ya Kagera,Mara,Shinyanga,Tabora na Singida ikiwa na lengo kuu la
kuileta Wizara ya habari,utamaduni,Sanaa na Michezo mikoani na wilayani
karibu na wadau.
0 comments:
Post a Comment