SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Sunday, April 24, 2016

MWANAMUZIKI NGULI WA MUZIKI WA ASILI YA KIKONGO PAPA WEMBA AFARIKI DUNIA

 
Gwiji la Muziki Wa Dansi Mwenye Asili Ya Kongo, Mwenye Sauti Tamu Ya Kuvutia Papa Wemba afariki dunia baada ya kuanguka akiwa jukwaani katika tamasha #FEMUA9 na baadae kukimbizwa hospitali na hatimaye kufariki dunia nchini Abidjan.

Mwanamuziki nguli wa Congo Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba maarufu kama Papa Wemba amefariki dunia huko Abidjan, Ivory Coast, usiku wa kuamkia leo.

Habari zilizotufikia hivi punde zinasema marehemu Papa Wemba amefia hospitali alikokimbizwa mara baada ya kuanguka na kupoteza fahamu wakati akiwa katika onesho jukwaani.

Papa Wemba alizaliwa June 14, 1949 huko Lubefu katika wilaya ya Sankuru nchini Congo. Alijipatia umaarufu sana kwa sauti nyororo na midundo ya Soukous ulimwenguni kote, ikiwamo Tanzania ambako amezuru mara kadhaa na kujizolea mashabiki wengi
.

 Papa Wemba akiwa jukwaani kwa mara ya mwisho jijini Abidjan, Ivory Coast, usiku wa kuamkia
 Papa Wemba aanguka na kupoteza fahamu katikati ya onesho
Wafanyakazi wa huduma ya kwanza wamepanda jukwaani. Hali ilizidi kuwa mbaya wakamkibiza hospitali ambako alikata roho.

0 comments:

Post a Comment