SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, March 23, 2016

SALIM ASAS AJITOLEA KUMUUNGA MKONO RAIS DR MAGUFULI JUU YA VITA DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA ,ASAIDIA KUHUDUMIA WAATHIRIKA WA DAWA ZA KULEVYA

Mlezi wa kituo hicho cha Iringa Sober Hous Bw Godwin Msillu kushoto akiwa na baadhi ya vijana waliokuwa watumiaji wa dawa za kulevya ambao wanaishi kituoni hapo .
Shadrack John ambae ni anaishi kituo cha Iringa Sober House aliyetoka mkoa wa Arusha akijisomea Biblia baada ya kuachana na matumizi ya dawa za kulevya .

Na MatukiodaimaBlog.

KAMANDA wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) mkoa wa  Iringa Bw Salim Asas ameunga mkono kwa vitendo mapambano ya vita dhidi ya madawa ya kulevya nchini yaliyoanzishwa na Rais Dr John Magufuli kwa kusaidia uanzishwaji wa kituo cha kusaidia waathirika wa madawa ya kulevya mkoani hapa.

Bw Asas ambae wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu alipata kuweka bayana mkakati wake wa kusaidia vijana walioathiriwa na matumizi ya madawa ya kulevya ameungana na kituo cha Iringa Sober House kilichopo Semtema katika Manispaa ya Iringa kuwasaidia vijana hao ambao afya zao zimeathiriwa na madawa ya kulevya kwa kuwakusana na kuwapatia tiba.

Akizungumza na mtandao wa matukiodaima leo Dr Alli Ngalla ambae ni Mkurugenzi wa NGOs ya Foundation for ellevition of drug eddiction anda sufferings (FADAS) wameanzisha kituo cha kutoa huduma kwa waathirika wa madawa ya kulevya cha Iringa Sober House ambacho kimeanza kufanya kazi chini ya ufadhili mkubwa wa Bw Asas .

Alisema kuwa kituo kituo hicho toka kimefunguliwa kina zaidi ya mwezi mmoja ambapo jumla ya wategemezi 7 ambao wanahudumiwa katika kituo hicho pamoja na wasimamizi watatu ambao pia walikuwa ni watumiaji wa dawa za kulevya ambao kwa sasa waliacha .

" Kwa kweli kuendelea kwa kituo hiki kumechangiwa kwa karibu na Salim Asas ambae amekuwa bega kwa bega kuona vijana walioathirika na madawa ya kulevya wanasaidiwa na anachofanya salim pia ni kumuunga mkono Rais Dr Magufuli ambae ametangaza vita dhidi ya madawa ya kulevya ......hivyo bado tunaomba wadau wengine kujitokeza kusaidia mapambano haya ya kunusuru afya za vijana wetu "alisema Dr Ngalla 

Kuwa lengo la kituo kuweza kuwahudumia waathirika wa madawa ya kulevya kutoka mikoa mbali mbali nchini hasa wamelenga kuwafikia vijana wa mkoa wa Mbeya, Njombe , Ruvuma na Iringa japo tafiti zinaonyesha mkoa wa Mbeya ndio unaongoza kwa matumizi ya madawa ya kulevya .Msimamizi wa kituo hicho Bw Godwin Msillu alisema kuwa mkakati wa kuanzisha kituo hicho ulitokana na mkakati wa NGOS ya FADAS ambao walikuja na mpango wa kuanzisha kituo hicho .

Alisema kuwa kati ya waathirika wa dawa za kulevya ambao wapo kituoni hapo baadhi yao ni kutoka mkoa wa Arusha na kuwa kumekuwepo na mafanikio makubwa kwa walengwa hao afya zao kuanza kuimarika na hivyo  kuwataka vijana wengine walioathirika na dawa za kulevya kutosita kufika kituoni hapo ili kusaidiwa zaidi.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake walioathirika na madawa ya kulevya Bw Shadrack John alisema kuwa amepata kufika mkoani Arusha kuja kupatiwa huduma hiyo na kuwa kwa sasa hali yake inaendelea vizuri zaidi.

Huku kijana Ibrahim Abdu alisema kuwa amekuwa akitumia madawa hayo kwa zaidi ya miaka 10 sasa kabla ya kuamua kuacha na kujiunga na kituo hicho hivyo kupongeza jitihada za Asas kuunga mkono kituo hicho huku akiwataka vijana wenzake kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya .

0 comments:

Post a Comment