Kumetokea
miripuko miwili katika uwanja wa ndege wa Zaventem mjini Brussels
Ubelgiji na mwengine katika kituo cha treni cha Maelbeek kulichopo
karibu na majengo ya taasisi za Umoja wa Ulaya.
Kwa
mujibu wa vyombo vya habari vya nchini humo, hadi sasa idadi ya watu
walioripotiwa kuwawa katika milipuko ya uwanja wa ndege wa Zaventem
imefika 13 wengine 35 wamejeruhiwa na kupelekwa hospitali. Usalama
umeimarishwa katia uwanja wa ndege huwo. Watu walioshuhudia tukio hilo
wamesema walisikia sauti za risasi pamoja na watu wakipiga kelele kwa
lugha ya kiarabau muda mfupi kabla ya kutokea milipuko hiyo.
Kwa
upande mwengine kumekuwa na taarifa za kukinzana juu ya mripuko wa kituo
cha treni, watu kumi wameripotiwa kuuwawa kwa mujibu wa shirika la
utangazaji la VTM la Ubelgiji, lakini bila ya kutoa maelezo zaidi, huku
vyanzo vyengine vikisema hamna aliyeathirka katika mlipuko huwo. Na
Shirika la utangazaji wa Umma la VRT nchini humo limesema mlipuko wa
uliotokea katika kituo cha reli ni wa kujitoa muhanga. Halikadhalika
mamlaka ya usafiri ya Ubelgiji imesema usafiri wote wa umma mjini humo
umesimamishwa ikiwamo wa reli na mabasi.
Waziri wa
mambo ya ndani wa Ubelgiji, Jan Jambon, ameitangaza nchi hiyo kuwa
katika hali ya hatari ya kiwango cha nne ambacho ndio cha juu kabisa.
Huku baraza la mawaziri nchini humo likiwa tayari limeitisha mkutano wa
dharura mara tu baada ya kutokea kwa mashambulizi hayo.
Usalama waimarishwa nchi kadhaa za Ulaya
Halikadhalika
serikali ya nchi hiyo inategemewa kukutana na waandishi habari
kuyazungumzia mashambulizi hayo. Waziri Mkuu wa Ubelgiji Charles Michel
ameandika katika ukurasa wake wa Twitter, kuwa serikali inafuatilia
kilahatua ya matukio hayo. Na kuongeza kwa sasa kipaumbele watapewa
walioathirika na wale ambao wapo katika uwanja wa ndege huwo, eneo la
mashambulizi.
Pamoja na
hayo, nchi kadhaa za Ulaya zimeimarisha usalama katika viwanja vya
ndege ikiwamo wa mjini Frankfurt hapa Ujerumani, Gatwick mjini London,
Uingereza pamoja na Charles De Gaulle mjini Paris Ufaransa.
Halikadhalika shirika la ndege la Aegean la Ugiriki limesitisha safari
zake zote zinazoelekea mjini Brussels.
Na kwa
upande wa Ufaransa rais wa nchi hiyo Francois Hollande ameitisha mkutano
wa dharura na Waziri wake Mkuu, Waziri wa Ulinzi pamoja na Waziri wa
mmabo ya ndani. Halikadhalika Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron
ameitisha mkutano na kamati ya dharura ya serikali nchini humo na kusema
nchi hiyo itasaidia vyovyote iwezanvyo.
Miripuko
hiyo inakuja siku chache baada ya kukamatwa kwa Salah Abdeslam mjini
Brussels, mshukiwa mkuu wa mashambulizi ya mjini Paris mwezi Novemba
mwaka jana ambapo watu 130 kuwawa.
0 comments:
Post a Comment