SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, February 11, 2016

MKUTANO WA 25 WA MWAKA WA WADAU NA WANACHAMA WAMFUKO WA PENSHENI WA PPF

  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashantu Kijaji (wa pili kulia) akimkabidhi Cheti za mshindi wa kwanza wajumla Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu Charles Kazuka, wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 25 wa mwaka wa Wadau na Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, ulioanza jijini Dar es Salaam, leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere,  unaomalizika kesho. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio (wa pili kushoto) ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Pensheni wa PPF, Ramadhani Kijjah. Picha na Muhidin Sufiani/Mafoto Media
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Pensheni wa PPF, Ramadhani Kijjah, akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano mkuu wa 25 wa mwaka wa Wadau na Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, ulioanza jijini Dar es Salaam, leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere,  unaomalizika kesho.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano mkuu wa 25 wa mwaka wa Wadau na Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, ulioanza jijini Dar es Salaam, leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere,  unaomalizika kesho.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashantu Kijaji (Mb) akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano wa 25 wa mwaka wa Wadau na Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, ulioanza jijini Dar es Salaam, leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere,  unaomalizika kesho. Akizungumza wakati wa mkutano huo Dkt.Kijaji aliupongeza Mfuko huo wa PPF kwa mikakati thabiti ya kutoa huduma zake kwaJamii. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE
 Baadhi ya Wadau na Wanachama wa Mfuko huowakimsikiliza Mgeni rasmi wakati wa ufunguzi huo leo kwenye Ukumbi wa  Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.
Baadhi ya Wadau na Wanachama wa Mfuko huowakimsikiliza Mgeni rasmi wakati wa ufunguzi huo leo kwenye Ukumbi wa  Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.
Baadhi ya Wadau na Wanachama wa Mfuko huowakimsikiliza Mgeni rasmi wakati wa ufunguzi huo leo kwenye Ukumbi wa  Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashantu Kijaji (wa pili kulia) akimkabidhi Cheti za mshindi wa pili wa Usafirishaji,Mawasiliano na Uzalishaji Umeme, Ofisa wa kampuni ya Simu za mkononi ya Airtel, Pamela Mwandetele, wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 25 wa mwaka wa Wadau na Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, ulioanza jijini Dar es Salaam, leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere,  unaomalizika kesho. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashantu Kijaji (wa pili kulia) akimkabidhi Cheti za mshindi wa kwanza wajumla Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu Charles Kazuka, wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 25 wa mwaka wa Wadau na Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, ulioanza jijini Dar es Salaam, leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere,  unaomalizika kesho. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio (wa pili kushoto) ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Pensheni wa PPF, Ramadhani Kijjah. Kulia ni Mjumbe wa kamati ya Bunge, Richard Ndasa.

Mgeni rasmi akitoa vyeti kwa washindi wamfuko huo...
Mwanachama wa PPF, Bakari Kaoneka, akitoa ushuhuda wa Fao la uzeeni , wakati wa ufunguzi wa mkutano huo.
Mwanachama wa PPF, Angela Mgulu, mfanyakazi wa Benki ya NBC ya jijini Mwanza, akitoa ushuhuda wa Fao la Uzazi , wakati wa ufunguzi wa mkutano huo.
Mwanachama wa PPF, Sarah Haule, mkazi wa Tabata jijini dar es Salaam, akitoa ushuhuda wa Fao la Uzazi , wakati wa ufunguzi wa mkutano huo.
Mwanachama wa PPF, Dereva wa Bodaboda kutoka Mkoa wa Mwanza, Lazaro Mussa, akitoa ushuhuda wa Fao la Wote Scheme wakati wa ufunguzi wa mkutano huo.
Wadau wakijisajili na kupewa 'Document' ili kuingia kushiriki mkutano huo...
Wageni wakivishwa Beji wakati wa zoezi la kujisajili ili kuingia ukumbini kuhudhuria mkutano huo.
Meneja wa Mfuko wa PPF,Lulu Mengele,akiwaelekeza jambo baadhi ya wakurugenzi ukumbini humo.
Sehemu ya wadau waMfuko huo ukumbini....
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, William Erio (kulia) akijadiliana jambo na Meneja Kiongozi wa PPF, Mbarouk Magawa (katikati) na mwendeshaji wa mkutano huo,Mc Mavunde
Wadau wa mkutano huo wakijadili jambo...
Wadau ukumbini humo....
Wadau wakisimama kumuaga mgeni rasmi baada ya ufunguzi huo...
Mkurugenzi Mkuu wa PPF,William Erio, akihojiwa na baadhi ya waandishi wa habari wa TV baada ya ufunguzi huo.
*********************************
SERIKALI imedhamiria kusimamia na kuhakikisha michango ya pensheni kwa
wafanyakazi wa Taasisi zinazopokea ruzuku kutoka serikalini inalipwa kwa wakati ili kuiwezesha mifuko ya hifadhi ya jamii kuwa na fedha ya kutosha kwa ajili ya uendeshaji na ulipaji wa mafao kwa wananchama.

Akifungua mkutano wa 25 wa mwaka kwa wananchama na wadau wa mfuko wa
pensheni wa PPF na wadau wengine wa hifadhi ya jamii katika Ukumbi wa
Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt.Ashatu Kijaji amesema Serikali inatambua umuhimu wa mifuko ya hifadhi ya jamii na tayari imeashaanza kulipa madeni ya serikali yanayodaiwa na mifuko.

“Tayari Wizara ya Fedha na Mipango imeshaagiza benki kuu kuandaa non-cash
bond ambayo itatolewa kwa mfuko ikiwa ni mkakati wa kulipa madeni hayo”
alisema Mhe.Dkt.Kijaji aliongeza kuwa serikali imetoa agizo la kuwataka waajiri wote kuhakikisha wana mikataba na wafanyakazi wao kwa kuwaandikisha katika mifuko ya hifadhi ya jamii na kuwachangia kama sheria inavyotaka.
“Naagiza kwamba hatua za kisheria zichukuliwe kwa kuwashitaki waajiri wote
wanaochelewesha michango na kuziomba mahakama kuzishughulikia mapema
kesi hizo ili kuondoa kero kwa wananchi na Mifuko” alisema Mhe. Dkt.Kijaji
Pia aliutaka mfuko wa PPF uangalie uwekezaji katika maeneo muhimu ambayo
hayapo katika mfumo uliopo sasa kwa kuzingatia kanuni za uwekezaji
zilizotolewa na Benki kuu ya Tanzania kwa kushirikiana na SSRA ili kujiongezea mapato.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamamini ya Mfuko wa Pensheni wa PPF
Bw.Ramadhani Khijjah ameeleza kuwa kwa sasa thamani ya mfuko imeongezeka kwa asilimia 40 kutoka shilingi trilioni 1.48 mwaka 2013 hadi kufikia shilingi trilioni 2.08 Juni 2015.
“Mfuko wa PPF umekuwa kimapato na kwa idadi ya wanachama ambapo mpaka mwishoni mwa mwaka 2015 thamani imeongezeka kwa kufikia kiasi cha shilingi trilioni 2.23” alisema Bw.Khijjah.

Aliongeza kuwa mbali na mafanikio hayo mfuko unakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ucheweleshwaji wa kulipwa kwa madeni ya mikopo mbalimbali, ucheweleshwaji wa michango ya wanachama unaofanywa na baadhi ya waajiri na kuongezeka kwa wanachama wanaoondoka kazini kabla ya umri.
Mkutano huo wa 25 wa mwaka kwa wanachama na wadau wa mfuko wa pensheni wa PPF ni wa siku mbili wenye kauli mbiu ya “ uendelezaji wa sekta ya hifadhi ya jamii umuhimu wa kuzingatia mabadiliko” utawawezesha wanachama kujadili mambo mbalimbali.

0 comments:

Post a Comment