Raisi wa Burundi Pierre Nkurunziza ambaye amerejea nchini mwake baada ya kushindikana kwa jaribio la mapinduzi ya kijeshi
Na Martha Saranga Amini
Raisi wa
Burundi Pierre Nkurunzizaamewatangazia raia wake kuwa sasa amani
imerejea nchini humo ikiwa ni siku tatu baada ya kushindwa kwa jaribio
la mapinduzi ya kijeshi.
Akihutubia
wananchi kupitia runinga Pierre Nkurunziza ametoa onyo juu ya jaribio
lingine lolote la kuchukua madaraka kwa nguvu litasababisha vita
umasikini na majanga yalikwisha onekana katika taifa hilo.
Hayo
yanajiri wakati Marekani ikitoa onyo hapo jana kwa raisi wa Burundi
Pierre Nkurunziza kuhusu kutowania muhula wa tatu wa uongozi kwa vile
kutazorotesha usalama nchini humo na kutishia misaada ya kimataifa.
Msemaji
wa Washington Jeff Rathke ameeleza kuwa Marekani inawasiwasi kufuatia
uwezekano wa kutokea ghasia zaidi baada ya raisi Nkurunziza kurejea
nchini Burundi.
Msemaji
wa washington amesema kuwa marekani bado inamtambua Nkurunzinza kama
raisi halali wa Burundi licha ya kusisitiza kiongozi huyo kutowania
muhula wa tatu.
Baadhi ya
maafisa wa kijeshi walioshiriki kuongoza mapinduzi wamekamatwa huku
wengine wakitokomea na kusakwa na majeshi tiifu kwa serikali akiwemo
kiongozi wa mapinduzi hayo Generali Godefroid Niyombare, ambaye awali
aliiambia AFP kuwa angejisalimisha kwa serikali.
0 comments:
Post a Comment