Picha ya pamoja
WATANZANIA
wametakiwa kuwa na utaratibu wa kuweka fedha zao benki hususani Benki ya NMB
kutokana na kuwa na promosheni ya Weka na ushinde ambapo wateja hujishindia
Bajaji, Pikipiki na baiskeli.
Wito
huo ulitolewa na Meneja wa NMB Kanda ya Mbeya, Lecrisia Makiriye, alipokuwa
akizungumza na wateja waliojishindia Bajaji, Pikipiki na Baiskeli kutoka Matawi
ya benki hiyo mkoani Mbeya.
Makiriye
alisema ni vema watanzania waendelee kuweka fedha kwenye akaunti zao ili
washinde kupitia matawi ya NMB zaidi ya 160 yaliyotapakaa nchi nzima kwa kupitia
mawakala wa tigo pesa na mpesa pamoja na NMB Mobile kupitia simu za mkononi.
Alisema
katika Droo ya nane iliyochezeshwa nchi nzima tayari wameshapatikana washindi
34 wa bajaji, 32 wa pikipiki na washindi wa baiskeli 264 ambapo alitoa wito kwa
wateja wengine kuendelea kuweka fedha kwenye akaunti zao.
Alisema
kwa Kanda ya Mbeya ina jumla ya washindi 26 ambapo washindi 3 walijipatia
Bajaji, washindi watatu wameshindia pikipiki na wateja 20 wamejipatia baiskeli
na kuongeza kuwa zimetengwa zaidi ya shilingi Milioni 500.
Mwisho.
|
0 comments:
Post a Comment