SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, November 14, 2014

Taarifa Kwa Umma Kutoka Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania -TRL Kuhusu Huduma ya 'Treni ya Mwakyembe'

Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania -TRL unasikitika kuwatangazia kuwa kuanzia leo jioni saa 10 hakutakuwepo huduma ya usafiri wa treni ya Jiji maarufu kama ' treni ya Mwakyembe' hadi siku Jumatatu Novermba 17, 2014 huduma itakaporejea kama kawaida.

Ufafanuzi wa sababu za kusitishwa huduma umeeleza kuwa kichwa kimojawapo ambacho hutoa huduma kimepelekwa Karakana Kuu ya Morogoro kwa ajili ya ukarabati maalum na kwamba kinatarajiwa kurejeshwa Dar es Salaam jioni ya siku ya Jumapili. Novemba 16, 2014 baada ya kukamilika zoezi hilo la ukarabati.

Huduma zitarejea tena siku ya Jumatatu saa 12:30 asubuhi kuanzia kama kawaida kituo cha Ubungo Maziwa.

Atakayesoma taarifa hii amwarifu mwenzake!
Uongozi wa TRL unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza!

Imetolewa na
 Afisi ya Uhusiano ya TRL
kwa Niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TRL
Mhandisi Kipallo Amani Kisamfu.
Dar es Salaam,
Novemba 13, 2014

0 comments:

Post a Comment