SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, November 1, 2014

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AFUNGUA MKUTANO WA 4 WA KITAIFA KUHUSU UBORESHAJI

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifungua mkutano wa 4 wa kitaifa kuhusu uboreshaji Viwango vya huduma ya Afya. Mkutano huo ulifanyika jana Octoba 31-2014 katika ukumbi wa mikutano wa Benki kuu ya Tanzania jijini Dar es salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikabidhi tunzo za waliofanya vizuri katika vigezo mbalimbali vya uboreshaji viwango vya huduma ya Afya kwa Mkurugenzi wa huduma za uuguzi Hospitali ya Bugando jijini Mwanza Sister Viola Mumishi Katika Mkutano wa 4 wa kitaifa kuhusu uboreshaji wa Viwango vya huduma ya Afya. Mkutano  huo ulifanyika leo Octoba 31-2014 katika ukumbi wa mikutano wa Benki kuu ya Tanzania jijini Dar es salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasikiliza wahudumu wa mfuko wa bima ya Afya NHIF alipotembelea mabanda ya maonesho kwenye  mkutano wa 4 wa kitaifa kuhusu uboreshaji Viwango vya huduma ya Afya. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Benki kuu ya Tanzania jijini Dar es salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipata maelezo kutoka kwa Afisa ustawi wa Jamii Damel Masunzu alipotembelea banda la Wizara ya Afya kwenye maonesho uboreshaji Viwango vya huduma ya Afya. Katika Mkutano wa 4 wa kitaifa kuhusu uboreshaji wa Viwango vya huduma ya Afya. Mkutano  huo ulifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Benki kuu ya Tanzania jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal katikati akiwa katika picha ya pamoja wa washiriki wa Mkutano wa 4 wa kitaifa kuhusu uboreshaji wa Viwango vya huduma ya Afya.

0 comments:

Post a Comment