SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Sunday, November 16, 2014

BINGWA WA KUCHEZA NA PIKIPIKI ATUA NCHINI LEO KUTOA BURUDANI COCO BEACH, DAR


MWANAMICHEZO ambaye anacheza kwa kutumia pikipiki Bian Capper kutoka nchini Afrika kusini ametoa wito kwa watanzania kucheza mchezo huo ambao mbali ya kufurahisha pia unatumia akili na kukufanya uwe mkakamavu wakati wote.
Akizungumza jana kabla kuonesha umahiri huo mchezaji wa pikipiki ambaye ni raia wa Afrika Kusini anayefanya ziara katika nchi za Afrika kwa udhamini wa kinywaji cha Redbull atakuwa nchini kwa ziara za ya maonesho ya kuonesha namna ya kucheza na pikipiki kwa siku tatu.
 Onyesho la kwanza lilianza jana kwenye viwanja vya Coco beach , leo Jumapili atakuwa Mlimani City na kesho Jumatatu atakuwa katika eneo la Ubungo Tanesco ambako litakuwa onyesho lake la mwisho.
Capper amesema kwamba amefurahia kuweza kufika nchini pia tayari ameshafanya maonyesho yake katika nchi za Kenya na Uganda.
Wakati huohuo Rais wa Tanzania Motorcross Acrobatic Club Blagina Mwihava alisema kwamba wamemleta mwanamuchezo huyo ambaye wana imani kubwa ataleta msisimko mkubwa kwa vijana wa kitanzania kuweza kupata hamasa ya kucheza mchezo huo wenye mvuto.
“Hii itakuwa ni shoo kwa watanzania ili waweze kuvutika kucheza mcheo huu wa aina yake .

Ziara ya mchezaji huyo imeratibiwa na Kampuni ya Mohans inayosambaza kinywaji cha Redbull nchini maonesho hayo yote ni ya wazi. 

PICHA ZOTE NA CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG

0 comments:

Post a Comment