Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota (Kushoto) akifafanua jambo katika mkutano wa wadau wa mawasiliano ya Tehama ujulikanao kwa jina la Capacity Africa. kampuni hiyo ni moja wa wadhamini wa mkutano huo. Kulia ni Mwakilishi wa kampuni ya internet solution Prenesh Padayachee.
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia January Makamba (Kulia)
akizungumza katika mkutano wa wadau wa teknolojia ya Tehama (Capacity
Africa 2014) ambapo amesema serikali itaondoa tatizo la mawasiliano
nchini na huku ikitarajia kusambaza huduma hiyo kwa vijiji 1,800 ifikapo mwakani na vijiji 4,000 ikikapo mwaka 2017. Kushoto kwa Naibu Waziri Makamba ni mkurugenzi wa kampuni ya Seacom Byron Clatterbuck na Mwakilishi wa kampuni ya internet solution Prenesh Padayachee.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Six Telecoms, Rashid Shamte akifafanua jambo kuhusiana na
maendelea ya teknolojia ya Tehama nchini. Kampuni hiyo ni moja ya
wadhamini wa mkutano huo unaofanyika nchini kwa mara ya pili. Kulia ni Ofisa Biashara mkuu wa kampuni hiyo, Tinashe Bgoya.
Ofisa
Biashara mkuu wa kampuni ya Six Telecoms, Tinashe Bgoya (kushoto)
akizungumzia maendeleo ya maendelea ya teknolojia ya Tehama nchini.
Kulia ni Saidi Mohmed Alli ambaye ni Mkuu wa kitengo cha ‘Data’ cha
kampuni hiyo.
***********
Na Mwandishi wetu, Dar
Dar
es Salaam. Jumla ya vijini 1,800 vinatarajia kupatiwa mawasiliano ya
simu ya na teknolojia ya mawasiliano ya habari na mawasiliano (Tehama )
ifikapo mwakani.
Akizungumza
katika ufunguzi wa mkutano wa wadau wa Tehama wa Africa (Capacity
Africa), Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia January
Makamba alisema kuwa mpango huo upo katika hatua za mwisho na ifikapo
mwaka 2017, jumla ya vijiji 4,000 zitakuwa vimepatiwa huduma hiyo.
Makama alisema kuwa serikali ipo katika hatua za mwisho kuzungumza na kampuni ya simu kutoka Vietnam ijulikanayo kwa jina la Viettel na hivi karibuni wanatarajia kuzindua rasmi mpango huo.
Alisema
kuwa kuna vijiji mbali mbali Tanzania havina kabisa mawasiliano na
jukumu la serikali kuhakikisha kuwa tatizo hilo linatatuliwa.
Kwa
mujibu wa Makamba sekta ya mawasiliano inazidi kukuwa na serikali
imeweka mpango maalum kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma hiyo
tena kwa ubora wa hali ya juu.
Alisema
kuwa sekta hiyo ina changamoto nyingi kutokana na kupanuka kwa
teknolojia ya mawasiliano na tayari serikali imechukua hatua kukabiliana
na tatizo hilo hasa baada ya kukamilika kwa hatua ya tatu ya mkongo wa
Taifa wa mawasiliano.
“Mpaka
sasa ni mkoa wa Simiyu tu haujafikiwa na mkongo wa taifa na hiyo
imetokana na kugawanywa kwa mkoa wa Shinyanga, hata hivyo mikakati
inafanyika ili kuhakikisha mkoa huo unapata huduma hiyo na kuanza
kufurahia huduma ya Tehama,” alisema Makamba.
Naye
Mkurugenzi wa kampuni ya Six Telecoms, Rashid Shamte alisema kuwa
anaamini kuwa kukamilika kwa mkongo wa Taifa kutanufaisisha nchi jirani
ambazo hazina bahari.
Shamte
ambaye kampuni yake ilidhamini mkutano wa mwaka 2012 alisema kuwa
wanafuraha kubwa kuona nchi inafanya juhudi za kutatua tatizo la
mawasiliano vijijini na nchi takribani nane zinazoizunguka Tanzania.
Ofisa
Mkuu wa Masoko na Mauzo wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota
alisema kampuni yao imeanzisha kitengo cha mtandao wa internet ambacho
kitatoa huduma hiyo kwa bei nafuu.
“Lengo
letu kubwa ni kurahisisha mawasiliano, hivyo tunawahikikishia kuwa watu
wote wanaoishi vijijini watapata huduma hii kwa bei nafuu,” alisema Ngota.
0 comments:
Post a Comment