Na Beatrice Lyimo- MAELEZO.Dar es salaam.
Wizara
ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo
inatarajia kufanya kampeni shirikishi ya ugonjwa wa Surua na Rubella
kuanzia tarehe 18 hadi 24 oktoba, 2014.
Akizungumzia
kampeni hiyo itakayofanyika nchini nzima leo jijini Dar es Salaam,
Kaimu Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt. Donan Mmbando amesema kuwa
itawahusisha watoto wenye umri wa kuanzia miezi 9 hadi miaka 15.
Amesema
kampeni hiyo itaambatana na utoaji wa matone ya Vitamini A, dawa za
kutibu na kukinga magonjwa ya Minyoo, Usubi,Matende na Mabusha.
Dkt.
Mmbando amesema kuwa lengo na madhumuni ya kampeni hiyo ni kudhibiti
milipuko ya magonjwa ya Surua na Rubella ili kupunguza vifo na madhara
yanayosababishwa na magonjwa hayo.
“Katika
kampeni hii tutatoa dawa za kutibu na kukinga magonjwa ya Minyoo,
Usubi, Matende na Mabusha katika mikoa 16 yenye maambukizi makubwa ya
magonjwa haya”, Amesisitiza Dkt. Mmbando.
Amefafanua
kuwa chanjo ya Surua na Rubella itatoa fursa ya kutoa kinga kwa watoto
wengi zaidi ambao hawakupata chanjo hiyo utotoni katika mikoa yenye
maambukizi makubwa ya magonjwa hayo ambayo ni Mtwara, Lindi, Tanga , Dar es salaam,Morogoro, Pwani, Tabora, Manyara, Iringa, Ruvuma, Rukwa, Katavi, Singida, Dodoma na Njombe.
Akitoa
ufafanuzi kuhusu chanjo hizo amesema kuwa chanjo ya Surua na Rubella
itatolewa kwa watoto wenye umri wa miezi 9 hadi chini ya miaka 15,
matone ya vitamin A kwa watoto wenye umri wa miezi 6 hadi chini ya miaka
5.
Nyingine
ni dawa za minyoo (Mebendazole) zitakazotolewa kwa watoto wenye umri wa
miezi 12 hadi chini ya miaka 5 nchi nzima na dawa za kutibu na kukinga
minyoo (Albendazole) Usubi, Matende na mabusha au Ngirimaji kwa watu
wenye umri wa kuanzia miaka 5 na kuendelea katika mikoa 16
iliyobainishwa.
Kwa upande wake Meneja Mpango wa Taifa wa Chanjo wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt.
Dafrosa Lyimo ametoa wito kwa wazazi kuhakikisha kuwa wanawapeleka
watoto wao katika vituo vya afya ili waweze kupata chanjo hiyo.
Pia
ametoa wito kwa mama wajawazito kuhakikisha kuwa wanapata chanjo ya
Surua-Rubella ili kuwakinga watoto wao dhidi ya matatizo ya Moyo, mimba
kuharibika, kujifungua kabla ya wakati na mtindio wa ubongo yanayotokana
na ugonjwa huo.
0 comments:
Post a Comment