Mgeni
rasmi Mama Tunu Pinda akisalimiana na Mwenyekiti wa TAWA UK Bi Mariam
Kilumanga , alipowasili katika Balozi zaTanzania Uingereza. Nyuma ya
Mama Tunu ni Mwenyeji wake Mama Joyce Kallaghe na pembeni Afisa Mkuu
Kiongozi wa Ubalozi Caroline Chipeta.
Mama Tunu Pinda akiweka sahihi kwenye kitabu cha wageni Ubalozini , huku mama Kalaghe akiangalia.
Mama
Tunu kati akiwa na Mwenyeji wake kushoto Mama Joyce Kallaghe na kulia
Mtoa Mada ya fursa na Uwekezaji aliyeambatana na mama Tunu Tanzania
Women Chamber of Commerce Mama Anna Matinde.
Baadhi ay Wanawake waliohudhuria wakimkaribisha Mama Tunu na Mama Matinde.
Katibu wa Tanzania Women Association Uk (TAWA UK ) Bi Mariam Mungula akiongea machache kuwakaribisha wageni.
Mama Joyce Kallaghe , ambaye pia ni Mlezi wa TAWA UK , akifungua Mkutano rasmi na kuwatambulisha wageni wake.
Mama
Anna Matinde akiongea na akina mama mambp mengi ya kusisimua na
kuhamasisha aliyokuwa nayo kuhusu Uwekezaji nyumbani Tanzania.
Baadhi ya akina mama wenye shauku kubwa wakimsikiliza mama Matinde kwa makini.
Mama Tunu Pinda aliposimama kuongea na akina mama na kufunga Mkutano.
baadhi ya Wakina mama washiriki wakipata picha na wageni rasmi.
Maafisa wa Ubalozi wanawake katika Picha ya upendeleo na wageni wao.
Wageni na Uongozi wa TAWA UK walioandaa Mkutano huo.
Mama
Tunu Pinda alikuwa Mgeni rasmi katika Mkutano cha akina mama wa
Kitanzania waishio Uingereza , Kilichoandaliwa na Kikundi cha Umoja wa
Wanawake kiitwacho Tanzania Women Association UK (TAWA UK).
Mama
Tunu Pinda alihudhuria Mkutano huo kwa mualiko wa mwenyeji wake Mrs
Joyce Kallaghe Mke wa Balozi wa Tanzania Uk, Peter Kallaghe.
Mtoa
mada aliyeongozana na Mama Tunu , alikuwa ni Mama Anna Matinde ,
mwanamke Mjasiriamali mahiri na aliyebobea ambaye ana kofia mbalimbali
za Uwakilishi wa Wanamke na kibiashara katika taasisi tofauti za sekta
Binafsi ikiwemo na kuwa Mkurugenzi wa Tanzania Women Chamber of
Commerce.
Mama
Matinde licha ya kuwatia moyo akina mama na kuwahamasisha wajikite
kwenye biashara Binafsi na kubadilishana Ujuzi kutoka Tanzania na
Uingereza, vilevile aliwapa somo la Uwekezaji na pamoja na kuainisha
Fursa nyingi za kuwekeza zilizopo nyumbani Tanzania. Baada ya kikao
wanawake wengi walioyeshwa kuridhika na ushauri wa mama Matinde.
Mgeni
rasmi Mama Tunu Pinda aliwahimiza akina mama vilevile wasisahau kuwekeza
nyumbani hat kama wako nje ya Nchi, na kuwahakikishia kwamba sasa hivi
mwanamke wa Kitanzania anaelekea kuwa na haki sawa za umiliki ardhi na
mali kama ilivyoainishwa katika Katiba Iliyopendekezwa endapo itapita
kwa wananchi, Hivyo aliwasihi akina mama hao wasiwe na woga wa kuwa na
mali kutokana na baadhi ya mila kwani Katiba itawalinda.
Mkutano
huu uliofana ulimalizika kwa ahadi ya Uongozi wa TAWA UK walioratibu
Kikao hiki kuwa watafanya Mkutano Mkubwa Zaidi wa Uwekezaji na Fursa kwa
Akina Mama Muda si mrefu.
0 comments:
Post a Comment