Staa wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel .
Stori: Imelda Mtema
STAA wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel,
amesema hakuna ukweli wowote wa yeye kutanua na Waziri wa Maliasili na
Utalii, Lazaro Nyalandu nchini Marekani, kwani alikutana naye ukumbini,
akiwa amealikwa na blog iitwayo Vijimambo ambayo hutangaza utalii wa
Tanzania nchini humo kila mwaka.GPL
Alisema
wakati wa safari yake hakuelewa lolote kuhusu Waziri Nyalandu na
anashangazwa na yanayozungumzwa hivi sasa kwani baada ya kumsalimia
walipokutana, hawakuwahi kuonana tena hadi aliporejea, kwani yeye
alikuwa amepangiwa kwenye hoteli ambayo pia ndiyo ukumbi wa shughuli
hiyo ulipokuwa.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akizungumza jambo.
“Watu
wanataka kunijengea uadui na mke wake Faraja Kota ambaye tunaheshimiana
sana, mimi nilialikwa kule nikiwa na wasanii wengine, wanamuziki Kassim
Mganga na IT na hata malipo ya kazi yangu nililipwa na wao, wanaosema
nilitumia hela za wizara sijui wanataka nini, kama wizara iliwapa fedha
hao waliotualika mimi sijui,” alisema muigizaji huyo.
0 comments:
Post a Comment