Vikwazo vya Umoja wa Ulaya dhidi ya Urusi vitaanza rasmi kutumika leo.
Hata
hivyo, vitaondolewa vyote au baadhi yake tu mwezi ujao iwapo kutakuwa
na maendeleo katika utekelezaji wa mpango wa amani wa Mashariki mwa
Ukraine.
Uamuzi wa kutekeleza vikwazo hivi ulifikiwa jana baada ya
mkutano wa pamoja kati ya waziri mkuu wa Uingereza David Cameron na
viongozi wengine mashuhuri wa EU.
Mchakato huu ulicheleweshwa kwa
siku kadhaa kwa hofu ya baadhi ya nchi kwamba vikwazo zaidi vitaharibu
matarajio ya kusitishwa mapigano.
Vikwazo hivi vipya vinayalenga makampuni ya mafuta ya Urusi, sekta za fedha na ulinzi.
Pia
wameongeza majina mengine 24 katika orodha ya maafisa wa Urusi na
viongozi wa waasi nchini Ukraine ambao wanakabiliwa na kunyimwa visa na
kuzuia mali zao.
HABARI NA BBC SWAHILI
HABARI NA BBC SWAHILI
0 comments:
Post a Comment