SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, September 12, 2014

RAIS KIKWETE HAWEZI KUAHIRISHA BUNGE

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, ambaye ni  Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania(TCD)Mhe. John Cheyo amesema kwamba mchakato mzima wa Katiba utamalizwa kwa kura ya maoni ya wananchi, hivyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Jakaya  Kikwete haiwezi kutamka leo kuliahirisha Bunge Maalum la Katiba kwa kuwa liko Kisheria.
 
Aidha Mhe. Cheyo alisema kilichoahirishwa ni mchakato wa kura ya maoni ya wananchi na si Bunge hilo kwa kuwa walikubaliana   katika kikao cha mashauriano, baina Rais Kikwete na  Viongozi  Wakuu wa Vyama vya Siasa vyenye wabunge vinavyounda TCD kuwa bunge hilo liendelee. 
 
Kauli hiyo imetolewa leo Bunge Mjini Dodoma na Mhe. Cheyo wakati wa mjadala wa kujadili sura zilizobakia za Rasimu ya Katiba Mpya, ambapo alisema hayo ndiyo makubaliano yaliyofikiwa.
 Aidha Mhe. Cheyo alisisitiza Katiba Mpya inayopendekezwa itakayopatikana itadumu kwa njia ya maridhiano.
 
“ Bunge hili linaendeshwa kwa mujibu wa sheria , Tangazo la  Serikali (Government Notice) Na 254 hili ndilo uhai wa Bunge hili hadi Oktoba 4, mwaka 2014, na wote tukakubaliana haiwezekani   Mhe. Rais akasema   leo Bunge likasitishwa.
 
“ Vitu viwili vikukutana  kwa nia ya maridhiano, vitu vingine vinaweza kuwekwa pembeni sawa na sasa na baadae vinaweza vinashughulikiwa kwa wakati huo,” alisema Mhe. Cheyo.
 
Mhe. Cheyo alisema anamwomba  Rais Kikwete atoe ruhusa ya kuwepo kwa kipindi maalum  cha kitakachorushwa na televisheni (video) ili kila mtu aonekana alichokisema, huku akionesha kusikitishwa na upotoshwaji wa makubaliano hayo, uliofanywa na baadhi ya wanasiasa.
 
 “ Mojawapo  ambayo tuliyokubaliana  Bunge hili lipate Katiba ambayo inapendekezwa na wananchi pia kwa hali tulinayo haiwezekani  mchakato mzima ukamalizika, mchakato utamalizika kwa kura ya maoni  ya wananchi. Kama tukifika  huko itabidi tuhairishe uchaguzi wa mwaka 2015.   Niliyoyasema  ndiyo makubaliano tuliyokubaliana,” alisisitiza.
 
Mhe. Cheyo alisema Rais Kikwete alikubali kukaa chini pamoja na TCD na hao wanaojiita Ukawa.
 
 Alisema  Rais Kikwete alifanya mazungumzo na  viongozi wa Vyama vya Siasa vyenye wabunge vinavyounda TCD  mara  kwa mara ya kwanza, Agosti 31, mwaka 2014 kwa saa nne na mara ya pili, Septemba 8, mwaka 2014 kwa  saa mbili. 
 
Kikao hicho cha mashauriano kilihusisha  kamati ya makatibu wakuu,  kamati ya wenyeviti wa vyama  vya CCM, CHADEMA,CUF na NCCR-  Mageuzi.
(Awadh Ibrahim)
Muingereza wa kwanza kupata maambukizi ya Ebola katika mlipuko wa sasa barani Afrika anatarajia kurejea katika nchi ambayo ndipo alipopata maambukizo ili kusaidiana na wenzake kupambana na ugonjwa huo.

Muingereza huyo William Pooley mwenye umri wa miaka 29 alitibiwa Jijini London baada ya kusafirishwa kwa ndege kutokea Sierra Leone baada ya kupata maambukizi ya ugonjwa huo hatari.

Baada ya kupatiwa tiba nyumbani Uingereza sasa Pooley amepona na kuruhusiwa kutoka hospitali na amesema anatarajia kurejea Sierra Leone katika wiki chache ili kusaidia tena kukabiliana na mlipuko wa Ebola.

0 comments:

Post a Comment