JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU TANZANIA
TANGAZO LA KUTENGENEZA NEMBO, RANGI, HERUFI NA KAULI MBIU
YA TAASISI
Wakala wa
Huduma za Misitu Tanzania ni wakala wa serikali unaojitegemea
ulioanzishwa chini ya Sheria ya Wakala namba 245 (Executive Agency Act
[Cap. 245]) na umeandikishwa katika Tangazo la Serikali (Government
Notice) Namba 269 iliyochapishwa kwenye Gazeti la Serikali la tarehe 30
Julai 2010.
Wakala wa
Huduma za Misitu Tanzania unahusika na shughuli za kiutendaji za
kuendeleza raslimali za misitu na nyuki zilizohifadhiwa kitaifa, misitu
ya kupandwa na misitu iliyoko nje ya hifadhi. Pia inahusika na kuboresha
mazao ya nyuki na kuendeleza hifadhi za nyuki na manzuki.
Lengo la
kuanzishwa kwa wakala huu ni kuboresha usimamizi na uhifadhi wa
raslimali za misitu na nyuki ili kuhakikisha upatikanaji endelevu wa
mazao na huduma bora za misitu na ufugaji nyuki kwa kushirikiana na
wadau wengine.
DIRA
Kuwa kielelezo cha uhifadhi bora na upatikanaji endelevu wa mazao na huduma za misitu na nyuki Tanzania.
DHAMIRA
Kusimamia
kwa misingi endelevu raslimali za misitu na nyuki kwa ajili ya
kuchangia katika mahitaji ya kijamii, kiuchumi, ki-ikolojia na
ki-utamaduni kwa kizazi cha sasa na kijacho.
MAJUKUMU YA WAKALA
o Kuanzisha na kuendeleza misitu ya hifadhi na hifadhi za nyuki za serikali kuu
o Kuanzisha na kuendeleza mashamba ya miti na manzuki za serikali kuu
o Kusimamia na kuendeleza raslimali za misitu na nyuki zilizoko kwenye ardhi ya jumla
o Kusimamia utekelezaji wa sheria za misitu na ufugaji nyuki katika maeneo yake ya usimamizi wa raslimali kisheria
o Kuelimisha umma kwa njia ya uenezi katika maeneo ya wakala
o Kuendeleza raslimali watu
o Kukusanya maduhuli yatokanayo na mazao na huduma za misitu na ufugaji nyuki
o Kulinda mali za wakala, na
o Kufanya biashara ya mazao na huduma za misitu na ufugaji nyuki
Hivyo,
Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, unakaribisha wabunifu wote wenye
uwezo, wakiwa kama binafsi au kampuni, kuleta kazi zao kwa ajili ya
kushindanishwa.
MATUMIZI YA NEMBO
Wazo hili
litagusa maeneo mbalimbali ya taasisi ikijumuisha na matumizi mapana
kwenye kazi za kila siku za taasisi. Kazi hii itatumika kuonesha sura
halali na kamili ya taasisi ikijumuisha maeneo yafuatayo:
o Nembo
Lazima Iwe rahisi kutambulika ambapo itatumika kwenye;
Ø Magari na vyombo vingine vya usafiri
Ø Majengo
Ø Mabango
Ø Business cards
Ø Stationeries
Ø Risit na Ankara,
Ø Mifuko na mabegi
Ø Vipeperushi
Ø Tovuti
Ø Tshirts
Ø TV graphics
Ø Na kwingine
o Kauli Mbiu
Ø Iwe ya kuvutia na ya maneno machache
o Rangi
Rangi itakayovutia na kujulikana kwa jina na namba kwenye computer kwa matumizi kwenye vifaa vifuatavyo na vinginevyo:
· Magari
· Nyumba
· Ofisi
· Sare
· Tshirts
o Herufi
Pendekeza aina ya herufi ya computer itakayotumika pamoja na ukubwa wake (Font type and size)
ANGALIZO
o Nembo ziwe kwenye nakala mbili moja ya rangi (coulored) na nyingine isiyo na yangi (Black and White).
o Kazi hii iletwe kwenye mfumo wa DVD/CD
o Nembo isipungue 5Mb na isizidi 10Mb
o Nembo iwe na tafsiri ya Kiswahili na Kiingereza
NAMNA YA KUTUMA
Mshiriki
alete kazi yake kwa EMS au barua iliyosajiliwa ndani ya bahasha
iliyofungwa vizuri ikiambatana na maelezo mafupi ya mchoro utakaoleta na
atume kwa anuani ifuatayo:
Mwenyekiti
Kamati ya Kutafuta Nembo ya Taasisi
WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU TANZANIA
Jengo la Mpingo
40 Barabara ya Julius Nyerere
15472
DAR ES SALAAM
Mshiriki
anatakiwa kutuma barua yenye kuonesha wazi anuani ya posta, simu na
baruapepe yake. Pamoja na barua hiyo, mshiriki aambatishe wasifu wake
binafsi na picha yake ya rangi.
TAREHE YA MWISHO YA KULETA KAZI
Mwisho wa kuleta kazi hii ni tarehe 5 Septemba, 2014. Mshindi atatangazwa ifikapo tarehe 15 Septemba, 2014.
Kazi hii itakuwa na zawadi ya shilingi milioni mbili kwa mshindi atakayepatikana.
Imetolewa na:
Mtendaji Mkuu
WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU TANZANIA
0 comments:
Post a Comment