Mfululizo wa milipuko ya gesi kusini
mwa Taiwan katika mji wa Kaohsiung imeuwa watu 24 na kujeruhi watu
270.
Milipuko hiyo imetikisa wilaya ya
mji huo ya Cianjhen, magari yaliyorushwa yamesambaa na
barabara zimepasuka na kuwa na mitaro.
Chanzo halisi cha kuvuja kwa gasi
hakijafahamika, lakini imefahamika kuwa milipuko hiyo imetokana na
kupasuka kwa mabomba ya gesi.
MMMMMM
Moto uliozuka baada ya milipuko ya gesi nchini Taiwan.
WATU 22 wamefariki dunia huku 270 wakijeruhiwa baada ya milipuko kadhaa iliyosababishwa na kuvuja kwa gasi kutokea katika jiji la Kaohsiung nchini Taiwan jana usiku. Mlipuko huo uliosababisha moto mkubwa uliopindua magari, kuharibu barabara na baadhi ya majengo.
Majeruhi makitolewa eneo la mlipuko.
Moto mkubwa ukiendelea kuwaka mtaa wa Kaohsiung nchini Taiwan
Magari, barabara vikiwa vimeharibiwa na milipuko hiyo.
Maafa zaidi yaliyosababishwa na milipuko hiyo.
0 comments:
Post a Comment