Viongozi
wa Jumuiya ya Watanzania DMV wakati wakimsubiri Rais Jakaya Mrisho
Kikwete Jumapili Julai 3, 2014 katika hoteli ya Marriot jijini
Washington DC
Viongozi
wa Jumuiya ya Watanzania DMV wakati wakimsubiri Rais Jakaya Mrisho
Kikwete Jumapili Julai 3, 2014 katika hoteli ya Marriot jijini
Washington DC
Viongozi
na wanachama wa Jumuiya ya Watanzania DMV wakati wakimsubiri Rais
Jakaya Mrisho Kikwete Jumapili Julai 3, 2014 katika hoteli ya Marriot
jijini Washington DC
Wajumbe wa Bodi ya Jumuiya ya Watanzania DMV
Rais Kikwete akimsalimia mmoja wa watoto waliokuwepo kumlaki
Rais Kikwete akilakiwa na wanajumuiya
Rais
Kikwete, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernad
Membe, Balozi wa Tanzania Marekani Mhe Liberata Mulamula na Bi Rose
Jairo, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora wakijadiliana jambo meza
kuu
Sehemu ya wanajumuiya na wageni toka sehemu mbalimbali wakiwa katika mkutano huo
Washiriki wa mkutano huo
Wanajumuiya wakiwa wametulia mkutanoni
Wanajumuiya
Wanajumuiya toka kila kona ya DMV na sehemu mbalimbali za Marekani
Sehemu ya viongozi wa Jumuiya na wanajumuiya
Wote wametulia wakifuatilia kinachoendelea
Wanajumuiya
Wanajumuiya
Wanajumuiya
Sehemu ya nyomi ya wanajumuiya
Wanajumuiya pamoja na baadhi ya viongozi
Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited,Bw Charles Singili akiongea na kunadi bidhaa mpya ya Diaspora Banking ambayo benki hiyo imeanzisha
Mwanajumuiya akiomba ufafanuzi wa maswala kadhaa yanayowasibu
Wanajumuiya wakifurahia jambo
Swali toka kwa mwanajumuiya
Wanajumuiya wakisikilia kwa makini kinachoendelea
Mwanajumuiya akiuliza swali
Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited,Bwa.Charles Singili akifafanua mambo kadhaa kuhusu Diaspora Banking
Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited,Bwa.Charles Singili akiendelea kutoa ufafanuzi
Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited,Bwa.Charles Singili akieleza faida za Diaspora Banking
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC),Julieth Kairuki akiongea
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC),Julieth Kairuki akifafanua jambo
Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV BW Iddi Sandaly akiongea
Rais Kikwete akifafanua jambo. Kushoto ni Mama Salma Kikwete na kulia ni Balozi Mulamula
Mtangazaji wa Clouds FM kipindi cha Power Breakfast Gerald Hand akirekebisha mitambo
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernad Membe akifafanua jambo
Rais
wa Jumuiya ya Watanzania DMV BW Iddi Sandaly akimtambulisha Bi Rose
Jairo, Kaimu Mkurugenzi wa Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa
Nyomi
Mawziri na wabunge waliohudhuria
Sehemu ya waliohudhuria

Rais Kikwete akihuytubia wanajumuiya wa DMV
Hotuba ikiendelea
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
amewataka Watanzania waishio nje ya nchi na wanaotaka kuona Tanzania
inakubali kuanzisha mfumo wa uraiapacha kutumia muda wao kujenga hoja za
jambo hilo badala ya kupoteza muda kwenye mijadala ya kwenye mitandao
ya jamii na blogu na kulaumu watu wengine.
Rais
Kikwete amewataka Watanzania hao kusema ili wasikike kwa sababu,
kimsingi, hoja ya uraiapacha haina nguvu miongoni mwa Watanzania
wanaoishi Tanzania bali hoja hii inatokana zaidi na msukumo wa
Watanzania wanaoishi nje ambao kwa bahati mbaya hawafanyi jitihada za
kutosha kutetea hoja yao.
Rais
Kikwete ameyasema hayo usiku wa Jumamosi, Agosti 2, 2014, wakati
alipokutana, akazungumza na kujibu maswali ya Watanzania wanaoishi
Marekani, hasa katika maeneo ya jiji la Washington D.C., na majimbo ya
Virginia, Maryland, New York na hata California katika mkutano
uliofanyika katika Hoteli ya Marriot Washington, mjini Washington D.C..
Rais
Kikwete yuko katika ziara ya siku tisa katika Marekani ambako miongoni
mwa mambo mengine atahudhuria Mkutano wa Kwanza wa Marekani na Afrika
ambao shughuli zake zinaanza kesho Jumatatu. Mkutano huo, umeitishwa na
Rais Barack Obama wa Marekani na unahudhuriwa na viongozi wan chi 47
kutoka Afrika.
Rais
Kikwete amewambia Watanzania hao kuacha kupoteza muda kujadili mambo
yasiyokuwa na maana na badala yake kuelekeza nguvu zao katika kujenga
hoja yenye nguvu zaidi ya uraiapacha, jambo ambalo ni moja ya mambo
yatakayojadiliwa katika mchakato wa Katiba mpya.
“Mnashinda
kwenye blogu mkijadili mambo ambayo wenzenu nyumbani wana uwezo mkubwa
zaidi kuyajadili kuliko nyie. Mnajiingiza katika mambo ambayo sisi
nyumbani tuna uwezo mkubwa nayo kuliko nyie. Kwa mambo haya, sisi
tunatosha zaidi. Mnaacha kujadili mambo yanayohusu maisha yenu – kama
hili la uraiapacha- na mnajiingiza katika mambo yasiyowahusu,” amesema
Rais Kikwete na kuongeza:
“Kwa sasa yupo huu mjadala wa uraiapacha mabo ni hoja yenu.
"Nyie
badala ya kushiriki katika mjadala huu kwa njia zote, mnashinda kujadili
mambo ambayo hayana maana. Kwanza hoja ya uraiapacha siyo hoja ya watu
wengi nyumbani, siyo jambo linalowahusu.Hata rasimu sina uhakika kama
mmeisoma vizuri na kujua nini kimependekezwa – lakini hata huo muda
hamna. Kazi yenu mnashinda mnajadili mambo yasiyokuwa na maana – nani
kavaa nguo fupi, nani kafanya nini, haya ndiyo mambo yanayochukua muda
wetu.”
Rais
Kikwete amesisitiza: “Ushauri wangu ni kwamba tumieni muda wetu kusaidia
kusukuma hoja yenu hii muhimu – ambalo kama mnavyojua limeingizwa
katika rasimu kwa mapendekezo ya CCM kwa sababu suala hilo haliwemo
katika rasimu ya kwanza.”







































































0 comments:
Post a Comment