Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti, Raphael Mwamoto akitoa maelezo ya huduma zinazotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Godfrey Zambi wakati alipotembea banda la Mfuko katika maonesho ya Nane Nane mkoani Lindi.
Meneja wa Mkoa wa Lindi, Fortunata Raymond akielezea namna Mfuko wa Afya ya Jamii unavyofanya kazi Mkoani humo.
Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Godfrey Zambi akisisitiza jambo baada ya kupata maelezo ya huduma za Mfuko huo ikiwa pamoja na kuupongeza kwa kazi nzuri.
Ofisa Mdhibiti Ubora wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Timothy Mwasajone akitoa ushauri wa namna ya kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza.
Sehemu ya wananchi wakisubiri kupata huduma katika banda la NHIF.
Ofisa Matekelezo Nicolous Mwangomo akitoa maelezo ya namna ya kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF).
Huduma ya upimaji shinikizo la damu ikiendelea.
Naibu Waziri akisikiliza ushuhuda wa wananchi wa namna wanavyonufaika na huduma nzuri za CHF.
=====
=====
SERIKALI
imeutaka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kuendesha huduma za elimu ya
kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza katika mikoa yote hususani vijijini
pamoja na upimaji wa afya bure ili wananchi watambue afya zao na
hatimaye kuongeza uzalishaji katika sekta za kilimo na uvuvi na biashara
kwa ujumla.
Agizo
hilo lilitolewa na Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Godfrey
Zambi wakati wa maonesho ya Nane Nane Kitaifa yanayoendelea mkoani Lindi
ambapo Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umeshiriki na unatoa huduma
mbalimbali zikiwemo za elimu kwa Umma, usajili wa wanachama, upimaji
afya bure ikiwemo saratani ya matiti.
Aidha
alisisitiza kuwa mbali na huduma hizo nzuri zinazotolewa na Mfuko, ni
vyema wananchi pia wakapata elimu juu ya umuhimu wa kujiunga na Mifuko
ya Afya ya Jamii ili wanapougua wapate matibabu bila ya usumbufu wowote.
“NHIF
mnafanya kazi nzuri sana nawapongeza, na hata huduma mliyoileta huku
Lindi katika kipindi hiki cha siku nane naamini wananchi wa maeneo haya
watanufaika na huduma hizi hususan ya upimaji wa afya bure, hivyo
ninachowaomba sasa ongezeni kasi hasa kwa kwenda vijijini ambako ndiko
kuna kundi kubwa la wananchi,” .
“Wakati
mkifanya hizi huduma pia wahamasisheni wananchi kujiunga na Mifuko hii
ya Afya ya Jamii ili wanapougua wapate huduma hata kama hawana fedha
mfukoni,” alisema Naibu Waziri.
Aidha
alitoa mwito kwa wananchi wa Mkoa wa Lindi, Mtwara na wananchi
wanaoishi jirani na mikoa hiyo kuhakikisha wanaitumia vyema fursa hii
wakati wa maonesho haya kufika katika banda la NHIF ili kupata huduma
ambazo zinatolewa bila malipo kwa wananchi lakini zimeghramiwa na Mfuko
wa Taifa wa Bima ya Afya.
Naye
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti Raphael Mwamoto, alisema kuwa NHIF kwa
sasa inaendesha huduma hizi katika mikoa yote kwa lengo la kuwafanya
wananchi kutambua umuhimu wa kujua afya zao lakini pia umuhimu wa kupata
huduma za matibabu kupitia Mifuko ya Afya ya Jamii.
Alisema
kuwa kwa upande wa elimu juu ya faida za kujiunga na Mifuko ya Jamii,
NHIF inao mpango wa elimu ya Kata kwa Kata ambayo inafanyika zaidi
katika maeneo ya vijijini ili kuwahamasisha wananchi kujiunga na
kunufaika na Mifuko hii.
“Mfuko
wa Taifa wa Bima ya Afya kwa sasa una ofisi zake kila Mkoa Tanzania
ikiwemo Ofisi ya Zanzibar, hivyo shughuli za elimu kwa umma na upimaji
wa afya za wananchi hufanywa mara kwa mara na maofisa wa Mfuko walioko
katika Ofisi zetu za mikoani” alisema.
Pia
Ndugu Mwamoto aliendelea kusema kwamba matumizi sahihi ya fedha za tele
kwa tele za CHF pamoja na fedha za matibabu zinazolipwa na NHIF katika
vituo vinavyotoa huduma kwa wanufaika wa CHF na NHIF ni jambo muhimu
sana. Alisema……..….’’
Fedha
zinazolipwa na Mfuko pamoja na CHF ni fedha nyingi ambazo zikitumika
vizuri zinaweza kuboresha huduma za afya hasa upatikanaji wa dawa maeneo
ya vijijini, kuna Halmashauri ambazo zimefanikiwa sana katika hili kwa
mfano Nachingwea, Iramba, Igunga. Zingine ni Halamsahauri za
Songea,Tanga ,Rombo,Singida na Mwanga. Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
unaziomba Halmashaouri zingine nchini kote ziige mfano huu’’,




0 comments:
Post a Comment