Hivi karibuni tumesikia Mlipuko wa Ugonjwa Hatari wa Ebola ambapo tayari umesharipotiwa kuua zaidi ya watu 1000 huko Guinea, Siera Lione, Liberia ...Na Juzi umeripotiwa Kuingia Nigeria......na Mpaka Sasa watu takribani 1750 wameripotiwa kuathirika na Ugonjwa huu.
SASA TUJIFUNZE KIDOGO
Ebola Ni Nini?
Ebola
ni ugonjwa wa Mlipuko ambao virusi vyake hushambulia mfumo wa Damu wa
Binadamu. Kwa Lugha ya Kisayansi Ebola huitwa haemorraghic fever,
Ugonjwa huu hupelekea Muathirika kuvuja damu sehemu karibu sehemu yoyote
ile ya mwili wake na hatimaye kusababisha kifo kutokana na muathirika
huyo kupoteza damu nyingi. Na Kuvuja Damu huko kunaweza kuwa ni ndani ya
Mwili au Nje ya Mwili.
Dalili
za Ugonjwa Wa Ebola huanza kuonekana siku mbili hadi wiki tatu mara
baada ya mtu kuambukizwa virusi hivyo na Kupelekea Homa, Muscle kuuma
pamoja na Kichwa Kuuma huku dalili zingine zikiwa ni Kutapika, kuharisha
kukifuatiwa sambasamba na Kupungua kwa ufanyaji kazi wa Ini na Figo
katika Mwili wa Binadamu.
Virusi Vya Ebola vinaweza kupatikana kwa kugusa damu au majimaji kwenye mizoga ya Wanyama hususani Nyani na Popo.
Vilevile
Popo anaaminika kubeba Virusi vya Ebola na kuvieneza bila ya yeye
kuhathiriwa na ugonjwa huo. Mara tu Binadamu anapokuwa na ugonjwa huo
basi ugonjwa huo unaweza kuenezwa kati ya binadamu na binadamu.
Udhibiti
wa Ugonjwa huu unaweza kudhibitiwa kwa kupunguza maambukizi kutoka kwa
Nyani walioathirika pamoja na Nguruwe kwenda kwa Binadamu.
Hii
inaweza kufanywa kwa Kuwaangalia wanyama hao kama wameathirika na virusi
hivyo kwa kuwaua wanyama hao endapo itabainika wameathirika na
kuteketeza kwa Umakini wa hali ya juu mizoga hiyo endapo ugonjwa
umebainika.
Vilevile
kuhakikisha Upikwaji mzuri na makini wa Nyama na kuvaa mavazi ya kuzuia
maambukizi kipindi unapojihusisha na Nyama kama vile Uchinjaji kunaweza
kuzuia maambukizi ya Ugonjwa huo.
Vilevile
uvaaaji wa Mavazi ya kuzuia Maambukizi kama Mask, kuosha mikoni kwa
maji safi na sabuni pia kunaweza kudhibiti maambukizi ya Ugonjwa Huo.
Endapo
itatokea kuna mtu ameathirika na ugonjwa huo hatari basi uangalizi wa
hali ya juu sana unatakiwa kipindi mgonjwa huyo anapewa matibabu au
huduma za afya ili kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo.
Hakuna matibabu maalumu (Specific treatment) ya ugonjwa huu mara unapotokea.
Ila
JItahada na huduma zinatakiwa kufanywa kwa mtu aliyeambukizwa ugonjwa
huu kwa kumpa either ORT - Oral Rehyadration Therapy yaani maji ya
kunywa yenye mchanganyiko wa sukari na chumvi.
Ebola
ni Ugonjwa ambao unasababisha idadi kubwa ya vifo na Asilimia 50 hadi 90
ya wagonjwa wa Ebola hupoteza maisha kutokana na Ebola.
Kwa Mara ya Kwanza ugonjwa huu uligundulika Nchini Sudan na Jamhuri ya Kidemokrasia Ya Kongo.
Ugonjwa huu umetokea kama Ugonjwa wa Mlipuko ambapo umetokea katika Ukanda wa Nchi zilizopo Sub Sahara katika Bara la Afrika.
Tokea
Mwaka 1976 mpaka 2013 takribani watu wasiozidi 1000 kwa mwaka
wanaambukizwa ugonjwa huu tokea ulipogundulika kwa mara ya kwanza.
Kadirio
Kubwa Kabisa la Mlipuko wa Ugonjwa huu unaoendelea kupoteza maisha ya
watu ni Mwaka 2014 Katika Nchini za Afrika Magharibi ambapo Ugonjwa huu
umeathiri Nchini za Guinea, Siera Lione, Liberia na Nigeria ambapo
Kenya imetahadharishwa kuwa nchi ambayo inaweza kupata maambukizi ya
Ugonjwa huo kutokana na Kuwa kitovu cha Safari za Kwenda na kurudi Nchi
za Afrika Magharibi.
Mwezi
Agasti Pekee takribani watu 1750 wameripotiwa kuathirika na ugonjwa huu
hatari japokuwa jitihada zinaendelea ili kutafuta chanjo ya Ugonjwa huu
huku kukiwa bado hakuna dawa yoyote iliyopatikana kwaajili ya Kutibu
Ugonjwa huu.
ZIFUATAZO NI DALILI ZA EBOLA:
HOMA
KICHWA KUUMA
KUHARISHA
KUTAPIKA
MWILI KUWA DHAIFU
MUSCLE NA JOINT KUUMA
KUUMA KWA TUMBO NA
KUPOTEZA HAMU YA KULA.
JINSI YA KUJIKINGA NA JANGA HILI LA EBOLA TUNASHAURIWA KUFANYA YAFUATAYO:
* KUNAWA MIKONO KWA MAJI SAFI NA SABUNI MARA NYINGI TUWEZAVYO
*KUEPUKA KUPEANA MIKONO NA WATU
*KUWA MAKINI NA MWANGALIFU KWA VYAKULA TUNAVYOKULA HUSUSANI NYAMA
*KUSAFISHA MAZINGIRA YETU NA KUPULIZIA DAWA ZA KUUA VIRUSI NA BACTERIA (FUMIGATE)
*KUVAA PROTECTIVE GEAR KAMA GLOVES, GUN BUTI NK
Unashauri
Endapo Unajihisi una dalili za Ebola au unahisi kuna mtu ana dalili za
Ebola basi toa ripoti haraka sana ili kuweza kupata huduma ya afya na
matibabu.
0 comments:
Post a Comment