Diwani wa
kata ya Ololosokwani na Mkurugenzi wa Irkiramat Foundation (RAMAT) Bw.
Yannick Ikayo Ndoinyo akiangalia kitanda cha kujifungulia wakimama
kwenye Zahanati ya Sero ambayo kwa siku inatibu wagonjwa 50 na zaidi
ikiwa na daktari mmoja huku wakazi wanaofuata huduma hiyo kutoka kata
hiyo na ya jirani Soitosambu kutembea umbali mrefu kwa Kilometa 7-15
kupata huduma ya afya.(Picha Zainul Mzige wa MOblog)
Na Mwandishi wetu, Ngorongoro
Wakazi wa vijiji vya Ololosokwan,
Soit-Sambu, Njoroi na Loipir kata za Ololosokwana na Soit-Sambu wilayani
Ngorongoro wanakabiliwa na changamoto kubwa ya huduma ya Afya kwa
kutembea umbali mrefu kufuata huduma hizo kwenye kijiji cha Sero huku
waathirika wakubwa ni kinamama na watoto.
Umbali wa zahanati hizo imekuwa sababu
kubwa ya vifo hususani kwa akina mama wajawazito wanaotaka kwenda
kujifungua na watoto halikadhalika wanapozidiwa hufia njiani kutokana na
umbali wa zahanati kutoka kijiji kimoja kwenda kingine wanapotakiwa
kuwahishwa hospitalini hali inayowafanya kutembea umbali mrefu kilometa
15 hadi kuipata huduma ya zahanati .
Akizungumza na waandishi wa habari
Diwani wa kata ya Ololosokwani na Mkurugenzi wa Irkiramat Foundation
(RAMAT) Yannick Ikayo Ndoinyo waliotembelea miradi inayofadhiliwa na
Shirika la Elimu na Sayansi (UNESCO) wilayani humo alisema serikali
haina budi kutimiza ahadi yake ya kujenga Zahanati kwa kila kata nchini
Tanzania kuwapunguzia wagonjwa hususan akina mama waja wazito na watoto
adha ya kutembea au kusafiri mwendo mrefu kutafuta huduma za afya.(Martha Magessa)
Ndoinyo alisema kuwa tatizo kusafiri
umbali mrefu kutafuta huduma ya afya lipo na kwamba vifo ya wamama na
watoto na kutopata huduma zinazotakiwa kwa wakati. Wananchi hupata
huduma za afya kutoka Sero ambayo ina umbali mrefu kutoka Ololosokwang
au wakati mwingine mgonjwa hupata rufaa rufaa hadi Hospitali ya wilaya
ya Waso na iwapo mgonjwa atakuwa katika hali mbaya ni tatizo.
Gari la
wagonjwa lilitolewa na serikali likiwa limeharibika kutoka na miundo
mbinu ya barabara na kushindwa kufanyiwa matengezo kwa muda mrefu hali
inayomfanya daktari wa Zahanati hiyo kuwafuata majumbani wagonjwa
mahututi kwenda kuwapatia huduma za afya.
“Utakuta
wagonjwa inabidi watembee umbali mrefu kwenda kupata huduma za afya
kwenye zahanati ya Sero hili ni tatizo tunaiomba serikali yetu
kuliangalia ili kuokoa vifo vya mama na mtoto”alisema diwani.
Ndoinyo
alisema kuwa pamoja na daktari kuwatembelea akina mama na watoto ili
kutoa huduma za afya majumbani kwao kumekuwa na changamoto mbalimbali
hususan vifaa vya vipimo vya kupima magonjwa mbalimbali.
Nae
Mkunga wa jadi Mama Naani alisema mtihani mkubwa unakuja pale wakati
mama mjamzito anapotaka kujifungua na anahitaji huduma ya ziada, hakuna
vifaa na kumlazimu mgonjwa au mama mjamzito kuembea umbali mrefu kupata
huduma hiyo hospitalini.
Madhumuni
ya ziara hiyo inayowashirikisha wawakilishi kutoka Kampuni ya Samsung
na mwakilishi kutoka ubalozi wa Uswiss hapa nchini ni kujionea miradi
mbalimbali inayoendeshwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni
(UNESCO) inayotekelezwa na redio ya Jamii Loliondo wilayani Ngorongoro.
Miongoni
mwa miradi inayofadhiliwa wilayani humo ni pamoja na Redio Loliondo
ambayo pia inafadhiliwa na kampuni ya simu za mikononi ya Airtel kwa
kurusha matangazo yake kupitia mnara wa kampuni hiyo na Mradi wa Maktaba
unaolenga kuwapatia wanafunzi uelewa wa mambo mbalimbali yanayohusu
masomo ya sayansi.
Afisa
Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph,
akishanga kitanda cha kujifungulia wakinamama kwenye zahanati hiyo
ambayo ina uhaba wa vifaa mbalimbali vya matibabu huku halmashauri
ikishindwa kumalizia majengo ya wodi kwa ajili ya kulaza wagonjwa ambapo
imeonyesha wakina mama na watoto wamekuwa wakifia njiani kutokana na
kutembelea umbali mrefu kufuata matibabu.
Vifaa
vinavyotumika kwenye zahanati hiyo wakati wakinamama wanapojifungua,
jingine ni Friji kwa ajili ya kuhifadhia chanjo mbalimbali za watoto na
kinamama linalotumia umeme wa jua.
Daktari
wa Zahanati ya Sero kata ya Ololosokwani Dkt. Veronika Nyoni (katikati)
akielezea changamoto mbalimbali anazokumbana nazo katika kutoa huduma
ikiwemo Umeme na kupelekea kutumia tochi wakati wakinamama
wanapojifungua ambapo ameiomba serikali kupitia wafadhili mbalimbali
kuwasogezea hata huduma ya umeme jua ili kukabiliana na changamoto
hizo.Kulia ni Mwanahabari wa gazeti la Zanzibar leo, Mahmoud Ahmad na
kushoto ni Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw.
Al Amin Yusuph wakimsilikiliza kwa makini Dkt. Nyoni.
Diwani wa
kata ya Ololosokwani na mkurugenzi wa Irkiramat Foundation (RAMAT) Bw.
Yannick Ikayo Ndoinyo akiwa na wadau wa maendelo wakiongozwa na UNESCO
waliofanya ziara katika kata ya Ololosokwani wilayani Ngorongoro.
Katikati ni Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw.
Al Amin Yusuph na kulia ni Meneja Mauzo wa Kampuni ya Samsung tawi la
Tanzania, Bw. Slyvester Nteere.
Nyumba ya
Daktari Mstaafu aliyekuwa akitoa huduma katika zahanati ya Sero zaidi
ya miaka 25 kama inavyoonekana ikiwa na Umeme wa jua pamoja na Dish
ikiwa ni maendeleo katika eneo hilo lililopo karibu na pori tengefu la
Loliondo.
0 comments:
Post a Comment