
Mwakalishi
wa Kampuni ya Simu ya TTCL Kanda ya Zanzibar Mohd Yussuf Mohd
akimfahamisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
mfumo mpya wa matumizi ya mawasiliano unaotumiwa na Kampuni hiyo kwa
wateja wake.
Afisa
Uhusiano msaidizi wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar Ispector Sharif Bakar
Sharif akimpatia ufafanuzi Balozi Seif juu ya mabadiliko ya pasi za
kusafiria ambayo yako katika kiwango cha teknolojia ya kisasa
Kimataifa.
********
Maonyesho
ya Biashara ya Iddi El Fitri yaliyoandaliwa na Wizara ya Baiashara
Viwanda na Masoko Zanzibar kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maendeleo ya
Biashara Tanzania { Tantrade } yanaendelea katiika viwanja vya Maisara
Mjini Zanzibar.
Taasisi
zisizopungua 67 kutoka Zanzibar na Tanzania Bara zikijumuisha zile za
mashirika ya Umma na Jumuiya zisizo za Kiserikali zimeshiriki maonyesho
hayo ya siku nne.

Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seid Ali Iddi alipata fursa ya
kutembelea maonyesho hayo katika siku yake ya tatu na kushuhudia bidhaa
mbali mbali za makampuni na wajasiri amali tofauti.

Balozi
Seif akiambatana na Naibu Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Mh.
Thuwaiba Kisasi,Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Nd. Julian Raphael pamoja na
baadhi ya watendaji wa Wizara hiyo alionyekana kuvutia na bidhaa hizo
jambo ambalo limekuwa kivutioa kwa baadhi ya wananachi walioonekana
kufurika katika eneo hilo.
Miongoni
mwa mabanda ya maonyesho aliyopata fursa kuyatembelea Balozi Seif ni
pamoja na Chama cha wafanyabiashara wenye viwanda na wakulima, Shirika
la Posta, Idara ya Uhamiaji, Vigor Turky Group na Zapeta.

Nyengine
ni Women Beam Light, Global Education Link, Princes Nadia Limited,
Morden Natural Herbal, Busara Promotion, Trust Natural Nutrition, Shumba
Cloves Foundation, Hoze Herbal Product, Ummy Vita, Zanto Food Product,
Digital City Limited pamoja na Meli Nne Herbal Product.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar







0 comments:
Post a Comment