Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Bw. Assah Mwambene (Kulia)
akibadilishana uzoefu na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bi. Joyce Mkinga (Kushoto) wakati
alipotembelea na kukagua Kitengo cha Mawasiliano Serikalini cha Ofisi
ya Rais, Tume ya Mipango.
Maafisa wa kutoka Idara ya Habari (Maelezo), Bw. Assah Mwambene (Kulia), ambaye ni Mkurugenzi wa Idara hiyo na Afisa Habari wa Idara hiyo, Bw. Frank Mvungi (Kushoto)wakiandika majina yao mara walipoingia kwenye Ofisi ya Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
Katibu
Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (Wapili
Kulia) akizungumza na Maafisa wa kutoka Idara ya Habari (Maelezo), Bw.
Assah Mwambene (Wapili Kushoto), ambaye ni Mkurugenzi wa Idara hiyo na Afisa HabAri wa Idara hiyo, Bw. Frank Mvungi (Kushoto) walipomtembelea Ofisini kwake. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bi. Joyce Mkinga.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Bw. Assah Mwambene (Kushoto) akizungumza na Katibu
Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (Kulia)
wakati wa ziara ya ukaguzi wa vitengo vya mawasiliano serikali.
Katibu
Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (Kulia)
akiagana na ugeni kutoka MAELEZO. Katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya
hiyo, Bw. Assah Mwambene na kushoto ni Afisa Habari wa Idara hiyo, Bw. Frank Mvungi.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Bw. Assah Mwambene (Kushoto)
akibalishana kadi za mawasiliano na Mkuu wa Kitengo cha Maktaba na
Nyaraka kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bw. Ally Msovu mara
alipotembelea Maktaba hiyo. Kwa mujibu wa taarifa za ubora wa Maktaba za
wizara za serikali hapa nchini, Maktaba hii ya Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango ni ya kipekee na ya kupigiwa mfano na imekuwa ikiwavutia wageni
wengi wa ndani na nje ya nchi wanaoitembelea Ofisi hii. Picha zote na Saidi Mkabakuli
*******
Na Saidi Mkabakuli
Katika
kutekeleza mkakati wa kutembelea na kukagua utendaji kazi wa vitengo
vya mawasiliano serikalini, Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Bw. Assah
Mwambene leo ametembelea Kitengo cha Mawasiliano Serikalini cha Ofisi ya
Rais, Tume ya Mipango, pia kuzungumza na Mtendaji Mkuu wa Ofisi hiyo,
Dkt. Philip Mpango.
Akiwa
katika ziara hiyo, Bw. Mwambene ambaye ndiye Msimamizi Mkuu masuala ya
Mawasiliano Serikalini na Msemaji wa Serikali amesema kuwa vitengo vya
mawasiliano serikali vina jukumu kubwa ya kuuelimisha umma wa Watanzania
juu ya masuala mbalimbali yanayojiri kwenye ofisi zao.
Bw.
Mwambene ameongeza kuwa lengo kuu la kuanzishwa kwa vitengo hivyo ni
kutoa elimu kwa umma na taarifa sahihi kwa Watanzania ambao ndiyo
waajiri wakuu wa watumishi wa umma nchini, hivyo watumishi wa vitengo
husika hawana budi kukidhi haja za Watanzania kwa kuwapatia taarifa
sahihi na kwa wakati.
“Tumieni
utaalamu wenu kwa kuwapatia taarifa sahihi na kwa wakati Watanzania ili
kuweza kutoa suluhu ya masuala mbalimbali ambayo munaweza kuyajibu,”
alisema.
Akizungumza
wakati alipokutana na Msemaji Mkuu wa Serikali, Katibu Mtendaji wa
Ofisi hiyo, Dkt. Philip Mpango, alimpongeza na kumshukuru Bw. Mwambene
kwa kutenga muda na kutembelea Tume ya Mipango, ambayo ndiyo Washauri
Wakuu wa Serikali katika menejimenti ya uchumi na masuala ya maendeleo.
Dkt.
Mpango aliweka bayana mkakati wa Ofisi yake wa kuwafikia Watanzania
wote bila kujali maeneo yao ya kijiografia kwa kuwaelimisha juu ya
mipango mbalimbali ya serikali yenye dhamira ya dhati katika kuwavusha
katika umaskini miongoni mwao.
“Tuna
mkakati wa kuwafikia na kuwaelimisha Watanzania juu ya masuala ya
mipango na maendeleo, na naomba kuchukua fursa hii kuiomba Ofisi yako
kutuunga mkono katika hili ili kuweza kufikia malengo ya Dira ya Taifa
ya Maendeleo (TDV) 2025,” alisema Dkt. Mpango.
Kwa mujibu wa TDV 2025 ni kuivusha Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
0 comments:
Post a Comment