Naibu
Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mwigulu
Nchemba ( Mb) akizungumza wakati wa majadiliano kuhusu masuala ya
Ushirikiano wa Kimaendeleo uliofanyika kwa siku mbili hapa Umoja wa
Mataifa. Mhe. Naibu Waziri alikuwa mmoja wa wanajopo wanne
walioendesha majadiliano hayo. Katika mchango wake, Naibu Waziri pamoja
na mambo mengine amesisitiza kuwa Ushirikiano wa Kimaendeleo bado
una mchango mkubwa katika ufanikishaji wa suala zima la maendeleo
endelevu lakini akataka iwemo mifumo ya ufuatiliaji ambayo itakuwa
jumuishi.
Mwakilishi
wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi
ambaye alifuatana na Mhe. Naibu Waziri katika mkutano huo. Aliyeketi
nyuma ya Balozi Manongi, ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiwano wa
Kimataifa, Balozi Celestin Mush na pembeni ya Balozi ni msaidizi wa
Naibu Waziri.
Huu
ni Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao kwa takribani wiki
mbili umekuwa ukihudhuria na kushiriki mikutano na mijadala mbalimbali
inayohusu mwelekeo wa ukamilishwaji wa malengo ya maendeleo ya
milenia ( MDGs), mchakato wa maandalizi ya ajenda na malengo mapya ya
maendeleo endelevu baada ya 2015 na Ushirikiano wa Kimaendeleo. Mikutano
hiyo imeandaliwa na Balaza la Umoja wa Mataifa linalohusika na
masuala ya Uchumi na Maendeleo ya Jamii ( ECOSOC)
Sehemu
ya washiriki waliokuwa wakifuatilia majadiliano hayo na ambapo baada
ya wanajapo kutoka mchango wao walipata fursa ya kuuliza maswali au
kuchangia maoni yao. Mkutano huu wa siku mbili kuhusu Ushirikiano wa
Kimaendelea umefanyika nchi na mwamvuli wa ECOSOC
Hii ni sehemu nyingine ya wajumbe walioshiriki majadiliano kuhusu Ushirikiano wa Kimaendeleo wakifuatilia majadiliano hayo
Na Mwandishi Maalum
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesisitiza kuwa Ushirikiano
wa Kimaendeleo bado ni eneo muhimu katika kuchagiza kasi ya maendeleo endelevu,
kupunguza umaskini na katika kuzijengea uwezo na mazingira ambayo hatimaye yataziwezesha nchi
zinazoendelea kupunguza utegemezi.
Hayo yameelezwa siku ya
Ijumaa na Naibu Waziri wa Fedha
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Mwigulu Nchemba ( Mb), wakati aliposhiriki akiwa mmoja wa wanajopo wanne
walioongoza majadiliano kuhusu hatua muhimu za kimataifa kuelekea 2015 ya mifumo ya ufuatiliaji na uwajibikaji kwa
ushirikiano wa kimaendelea.
Ajenda hii ilikuwa kati ya
ajenda kadhaa, ambazo mawaziri,
wabunge, wasomi, wafafiti na wajumbe kutoka
Taasisi zisizo za kiserikali
wamekuwa wakizijadili na kubadilishana
mawazo katika mkutano wao wa siku
mbili kuhusu Ushirikiano wa Kimaendeleo
( DCF). Mkutano huo ambao hufanyika
kila badaa ya miaka
miwili umefanyika chini ya
mwamvuli wa Baraza la
Umoja wa Mataifa linalohusika na Masuala
ya Uchumi na Maendeleo ya Jamii ( ECOSOC).
Akitilia mkazo kuhusu
eneo hilo la ushirikiano wa kimaendeleo, Naibu Waziri amewaeleza washiriki wa
majadiliano hayo kuwa uanzishwaji upya
wa ushirikiano kwajili ya maendeleo baada ya 2015 unatakiwa kuendelezwa
kama ulivyoainishwa katika lengo la nane
la MDGs ambalo linasisitiza kuhusu ushirikiano wa kimataifa kwa maendeleo.
Akaongeza kuwa
ushirikiano huo lazima pia ujengekee katika mazingira ya kuaminiana, kuwajibika na kuwa
na mifumo ya ufuatiliaji.
Akizungumzia kuhusu misaada ya maendeleo
( ODA) Naibu Waziri wa Fedha, amesema
ingawa misaada hiyo ya maendeleo bado ni muhimu hususani kwa nchi
zinazoendelea lakini mchango wake si
mkubwa sana katika eneo la maendeleo kwa ujumla wake.
Akabainisha pia kuwa
pamoja na nafasi yake katika ushirikiano
wa kimaendeleo upatikanaji wa ODA
umekuwa hautabiliki au kupatikana kwa wakati, na kikubwa zaidi hakuna mifumo
ya kuwawajibisha watoaji wa ahadi hizo
pale wanapokwenda kunyume na ahadi zao.
Na kwa sababu hiyo
akasema ushirikiano mpya wa kimaendeleo
lazima pia uimarishe pamoja na mambo
mengine uwajibikaji wa washirika wa
maendeleo na uanzishwaji wa vyanzo vipya
vya ugharimiaji wa maendeleo vitakayoziba pengo la misaada ya maendeleo kutoka nje.
Akataja maeneo
ambayo yanaweza kuzalisha
mapato mapya ya ndani kuwa
ni pamoja na ukusanyaji wa kodi na
udhibiti wa fedha chafu.Na kusisitiza
kwamba, ni kwa uimarishaji wa vyanzo hivyo vya mapato, udhibiti wake,
uwajibikaji pamoja na ushirikiano wa kimaendeleo ndipo mataifa yanayoendelea
yataweza kupunguza utegemezi wa misaada kutoka nje.
Kuhusu eneo la ufuatiliaji na uwajibikaji, Naibu Waziri amesema, Tanzania
siyo tu inafanya vema katika eneo
hilo lakini pia imejiwekea sera, taratibu na mifumo inayosimamia utawala bora na uwajibikaji.
Akatoa mfano uamuzi
wa Serikali wa kuiwasilisha Bungeni taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kama eneo mojawapo la
uwajibikaji.
Aidha akasema, kama hiyo haitoshi Tanzania, ni kati ya nchi ambazo kwa hiari yake iliamua
kujiunga na Mpango wa Uendeshaji wa Shughuli za Serikali kwa Uwazi ( OGP) kama
sehemu ya uwajibikaji .
Katika majadiliano
hayo, Naibu Waziri wa Fedha amesisitiza
pia haja na umuhimu wa nchi kumiliki na
kuendesha mambo yake yenyewe ikiwamo miradi ya maendeleo.
0 comments:
Post a Comment