Mgeni
rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mh. Mathias Chikawe
akisalimiana na Mkurugenzi Mkazi wa WFP nchini Bw.Richard Ragan
(katikati) mara baaada ya kuwasili kwenye hafla fupi ya kukabidhi msaada
wa dola za kimarekani milioni 1.4, kwa shirika la Chakula duniani (WFP)
kwa ajili ya kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu mkoani Kigoma. Kulia ni
Balozi wa Japan nchini, Mh. Masaki Okada. Picha na Zainul Mzige
******
Na Mwandishi wetu
Serikali
ya Japan imetoa msaada wa dola za kimarekani milioni 1.4, kwa shirika
la Chakula duniani ili liweze kuwasaidia wakimbizi zaidi ya 70,000
wakiwemo watoto 14,000 wanaohitaji Chakula katika kambi ya Wakimbizi
ya Nyarugusu mkoani Kigoma.
Akikabidhi
msaada huo, Balozi wa Japan nchini, Masaki Okada, aliwashukuru
wafanyakazi wa shirika la Chakula duniani wanaofanya kazi Tanzania kwa
kusaidia hali ya maisha ya Wakimbizi katika kambi zao.
Akizungumza
katika halfa hiyo, Okada alisema nchi jirani na Tanzania zimekuwa
katika vita zilizosababisha machafuko, lakini Tanzania kwa upande wake
imekuwa ikiwapokea kwa wema Wakimbizi hao hivyo inapaswa kuungwa mkono
kusaidia tatizo hilo la Wakimbizi
Balozi
Okada alikabidhi pia tani 91 za mafuta ya kupikia, tani 367 za Unga wa
nafaka, tani 400 za Maharage na tani 444 za Mahindi.
Kwa
upande wake Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani hapa nchini
Richard Ragan aliishukuru serikali ya Japan kwani imekuwa ikisaidia
Wakimbizi kwa miaka mitano iliyopita.
Mgeni
rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mh. Mathias Chikawe (katikati)
akibadilishana mawazo mara baada ya kuwasili kwenye Bandari ya Dar na
Mkurugenzi Mkazi wa WFP nchini Bw.Richard Ragan (kulia) pamoja na Balozi
wa Japan nchini, Mh. Masaki Okada.
********************************
Alifafanua
kuwa msaada huo utasadia watu 70,000, wakiwemo watoto chini ya umri wa
miaka mitano ambao idadi yao inakadiriwa kufikia 14,000 na akina mama
wajawazito wanaokadiriwa kufikia 3,150.
Alisema
kuwa pesa hizo zitasaidia pia ukuaji wa uchumi wa Tanzania kwani
Maharage zaidi ya tani 400 yatanunuliwa humu nchini. Alibainisha kwamba
kwa mwaka uliopita shirika hilo limetumia zaidi ya dola milioni 10 za
kimarekani kununua chakula kwa ajili ya wakimbizi hapa nchini.
Mshereheshaji
wa hafla hiyo Afisa Habari wa WFP, Fizza Moloo akiwakaribisha wageni
waalikwa kwenye halfa hiyo iliyofanyika jana jijini Dar kwenye Bandari
ya Dar es Salaam.
*************************
Akizungumza
kwa niaba ya serikali ya Tanzania, Waziri wa mambo ya ndani ya nchi,
Mh. Mathias Chikawe aliwashukuru wafadhili wote ambao wamekuwa
wakisaidia wakimbizi kwa miaka mingi.
“ninawashukuru
wote kwa pamoja kwa misaada yenu kwa kusaidia tatizo la wakimbizi
nchini kwetu kwa roho moja jambo linalomaanisha tunasaidiana katika
kuubeba huu mzigo” alisema Chikawe.
Hata
hivyo Chikawe alisema serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na jumuiya
za kimataifa imekuwa ikitoa misaada ya kuwarejesha Wakimbizi makwao hali
ya vita ikitulia na kwa kipindi cha zaidia ya miaka kumi serikali
imewarejesha wakimbizi zaidia ya laki sita.
Aliahidi
kuwa serikali ya Tanzania itaendelea kutafuta suluhisho la kusaidia
Wakimbizi, huku akiwahakikishia wafadhili kuwa milango ipo wazi
waendelee kutoa ushirikiano kwa mujibu wa tamko la Geneva la mwaka 1951.
Mgeni
rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mh. Mathias Chikawe akisoma
hotuba yake kwenye sherehe fupi ya kukabidhiwa msaada wa Chakula kwa
ajili ya kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu mkoani Kigoma uliotolewa na
Serikali ya Japan.
Balozi wa Japan nchini, Mh. Masaki Okada akisoma risala wakati sherehe
fupi za kukabidhi msaada wa Chakula kwa Serikali ya Tanzania
zilizofanyika kwenye Bandari ya Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani nchini (WFP), Bw. Richard Ragan
akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa (hawapo
pichani) wakati hafla fupi ya makabidhiano ya Chakula cha msaada
kilichotolewa na Serikali ya Jaapa kupitia Balozi wake hapa nchini.
Balozi
wa Japan nchini, Mh. Masaki Okada akikabidhi msaada huo kwa Mgeni rasmi
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mh. Mathias Chikawe (katikati) pamoja
na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani nchini (WFP), Bw.
Richard Ragan (kulia) kwenye hafla fupi iliyofanyika jana jijini Dar.
Kaimu
Meneja wa Bandari Bw. Nelson Mlali (kulia), Kaimu Afisa Mkuu wa
Mawasiliano Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Peter Millanzi 9katikati) na
Bw. David Mbonika wa WFP (kushoto) wakishuhudia tukio hilo.
Sehemu ya waandishi wa habari na wafanyakazi wa Bandari waliohudhuria halfa hiyo.
Mgeni
rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mh. Mathias Chikawe akifafanua
jambo kwa waandishi wa habari mara baada ya kupokea msaada huo kwenye
hafla fupi iliyofanyika jana jijini Dar. Kushoto ni Balozi wa Japan
nchini, Mh. Masaki Okada na Kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la
Chakula Duniani nchini (WFP), Bw. Richard Ragan.
Afisa
Uhusiano na Siasa Ubalozi wa Ujerumani, Bw. Benedict Kikove (katikati)
akijadiliana jambo na Afisa Habari wa WFP nchini, Bi.Seetashma THAPA
(kulia) na Mtafiti na Mshauri wa masuala ya uchumi wa Ubalozi wa Japan
nchini, Bi. Tamaki Yoshida mara baada ya tukio hilo.
Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani nchini (WFP), Bw. Richard Ragan
(kushoto) akifurahi jambo na Bw. David Mbonika wa WFP (kulia) pamoja na
Brian Mahemba wa African Marine Surveyors and Consultant Ltd. (katikati)
mara baada tukio hilo.
Baadhi
ya wafanyakazi wa Bandari wakiandaa msaada huo tayari kupakiwa kwenye
gari kupelekwa kwenye kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu mkoani Kigoma.
Forklift ikiingiza sehemu ya msaada huo kwenye Lori maalum lililoandaliwa kusafirisha mzigo huo.
Pichani juu ni sehemu ya msaada huo uliokabidhiwa jana jijini Dar es Salaam kwenye hafla fupi iliyofanyika Bandari ya Dar.
0 comments:
Post a Comment