SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Sunday, June 8, 2014

PPF yadhamini sherehe za siku ya Wazazi ya sekondari za Marian,Bagamoyo

Eliamini Amon Urio, (Katikati), mzazi wa Eileen, ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha tatu shule ya sekondari ya wasichana, Marian, iliyoko Bagamoyo mkoani Pwani, akielezea jinsi fao la elimu litolewalo na Mfuko wa Pensheni wa PPF, linavyosadia kumsomesha motto wake, baada ya kumpoteza mumewe mwaka 2005. Aliyasma hayo wakati wa sherehe za siku ya wazazi ya shule hiyo, Jumamosi Juni 7, 2014. Kushoto ni Meneja Uhusiano na Masoko wa PPF, Lulu Mengele na kulia ni Afisa Michango wa PPF, Kanda ya Kinondoni, Kwame Temu.
Joyce Nachenga, (Kusho), mwakilishi wa Mfuko wa PPF, Kanda ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, akiwaeleza wazazi wa wanafunzi wa shule ya sekondari Marian, faida za kujiunga na Mfuko huo, wakati wa sherehe za siku ya wazazi iliyofanyika shuleni hapo Jumamosi Juni 7, 2014.
Mmoja wa wanafunzi wanaofaidika na fao la Elimu, litolewalo na Mfuko wa Pensheni wa PPF, Rosalia Faustin Madulu, (Kulia), akieleza jinsi yeye binafsi ambaye kwa sasa yuko kidato cha Kwanza shule ya sekondari Marian iliyoko Bagamoyo, jinsi anavyofaidika na fao hilo tangu apoteze mzazi wake miaka 9 iliyopita. Aliyasema hayo wakati wa siku ya wazazi ya sekondari hiyo, Jumamosi Juni 7, 2014.Wakwanza kushoto ni Meneja Uhusian na Masoko wa PPF, Lulu Mengele, na wengine ni wanafunzi wengine wa shule hiyo wanaofaidika la fao hilo, Deborah Kibona, (Wapili kushoto) na Eileen Amon Urio
Meneja Uhusiano na Masoko wa PPF, Lulu Mengele (Katikati), akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya sherehe ya siku ya wazazi ya shule ya sekondari ya Marian huko Bagamoyo, mkoani Pwani Jumamosi Juni 7, 2014. Wanafunzi kadhaa wanasomeshwa na PPF, kupitia mpango wa Fao la Elimu litolewalo na Mfuko huo, mwanachama anapofariki. Kushoto ni Eliamini Amon Urio, ambaye motto wake, Eileen, alieko kidato cha tatu anasomeshwa na PPF, kupitia mfumo huo.
Meneje Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele (Wapili kushoto), akizungumza na wazazi na wanafunzi wa shule ya sekondari Marian, wanaosomeshwa na Mfuko huo kupitia mpango wa Fao la Elimu, wakati wa sherehe za siku ya wazazi ya shule hiyo, iliyoko Bagamoyo mkoani Pwani, Jumamosi Juni 7, 2014.
Meneja Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele, akitoa mada kuhusu faida mbalimbali zipatikanazo ukiwa mwanachama wa Mfuko huo,hususan Fao la Elimu, linalotolewa kwa watoto wa Mwanachama wa Mfuko huo aliyefariki dunia, wakati wa sherehe za siku ya wazazi ya shule ya sekondari Marian huko Bagamoyo, mkoani Pwani Jumamosi Juni 7, 2014. PPF ilidhamini siku hiyo. Kulia ni Mtoto anayefaidika na Fao la Elimu, mwanafunzi wa kidato cha kwanza, wa shule hiyo, Rosalia Faustin Madulu.
Mwadawa Hida, (Katikati), mzazi wa Rosalia Faustin Madulu, ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha Kwanza, shule ya sekondari ya wasichana, Marian, iliyoko Bagamoyo mkoani Pwani, akielezea jinsi fao la elimu litolewalo na Mfuko wa Pensheni wa PPF, linavyosadia kumsomesha motto wake, baada ya kumpoteza mumewe mwaka 2005. Aliyasema hayo wakati wa sherehe za siku ya wazazi ya shule hiyo, Jumamosi Juni 7, 2014. Kushoto ni Meneja Uhusiano na Masoko wa PPF, Lulu Mengele na kulia ni Afisa Michango wa PPF, Kanda ya Kinondoni, Kwame Temu.
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Kanisa Katoliki, Muadhama Policarp Kadinali Pengo,akinzungumza wakati wa sherehe za siku ya wazazi ya shule ya sekondari ya wasichana, Marian, iliyoko Bagamoyo mkoani Pwani, Jumamosi Juni 7, 2014.
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Kanisa Katoliki, Muadhama Policarp Kadinali Pengo, akimshukuru Meneja Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele, kutokana na Mfuko huo kudhamini sherehe za siku ya Wazazi ya sekondari za Marian, huko Bagamoto, mkoani Pwani Jumamosi Juni 7, 2014.
Deodatus Balile, akitoa mada kuhusu faida na umuhimu wa kuweka akiba kupitia mfuko ya Pensheni wa PPF, wakati wa sherehe za siku ya wazazi ya shule ya sekondari Marian, huko Bagamoyo, mkoani Pwani Jumamosi Juni 7, 2014.
Mmoja wa wanafunzi wanaofaidika na fao la Elimu, litolewalo na Mfuko wa Pensheni wa PPF, Rosalia Faustin Madulu, (Kulia), akieleza jinsi yeye binafsi ambaye kwa sasa yuko kidato cha Kwanza shule ya sekondari Marian iliyoko Bagamoyo, jinsi anavyofaidika na fao hilo tangu apoteze mzazi wake miaka 9 iliyopita. Aliyasema hayo wakati wa siku ya wazazi ya sekondari hiyo, Jumamosi Juni 7, 2014.Wakwanza kushoto ni Meneja Uhusian na Masoko wa PPF, Lulu Mengele, na wengine ni wanafunzi wengine wa shule hiyo wanaofaidika la fao hilo, Deborah Kibona, (Wapili kushoto) na Eileen Amon Urio.
Baadhi ya wazazi wakisikiliza mada zilizokuwa zikitolewa kuhusu faida za kujiunga na Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakati wa sherehe za siku ya wazazi ya shule ya sekondari Marian, iliyoko Bagamoyo mkoani Pwani Jumamosi Juni 7, 2014.