SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.
Showing posts with label BAGAMOYO. Show all posts
Showing posts with label BAGAMOYO. Show all posts

Sunday, June 8, 2014

PPF yadhamini sherehe za siku ya Wazazi ya sekondari za Marian,Bagamoyo

Eliamini Amon Urio, (Katikati), mzazi wa Eileen, ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha tatu shule ya sekondari ya wasichana, Marian, iliyoko Bagamoyo mkoani Pwani, akielezea jinsi fao la elimu litolewalo na Mfuko wa Pensheni wa PPF, linavyosadia kumsomesha motto wake, baada ya kumpoteza mumewe mwaka 2005. Aliyasma hayo wakati wa sherehe za siku ya wazazi ya shule hiyo, Jumamosi Juni 7, 2014. Kushoto ni Meneja Uhusiano na Masoko wa PPF, Lulu Mengele na kulia ni Afisa Michango wa PPF, Kanda ya Kinondoni, Kwame Temu.
Joyce Nachenga, (Kusho), mwakilishi wa Mfuko wa PPF, Kanda ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, akiwaeleza wazazi wa wanafunzi wa shule ya sekondari Marian, faida za kujiunga na Mfuko huo, wakati wa sherehe za siku ya wazazi iliyofanyika shuleni hapo Jumamosi Juni 7, 2014.

Monday, January 20, 2014

Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad afungua rasmi kampeni za uchaguzi wa madiwani, Bagamoyo

 Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akiwahutubia wafuasi na wapenzi wa chama hicho katika mkutano wa kampeni za udiwani uliofanyika kata ya Magomeni Wilayani Bagamoyo.

Tuesday, August 7, 2012

RAIS KIKWETE AHUDHURIA MAZISHI YA SHEKHE MKUU WA KIJIJI CHA MSATA, BAGAMOYO, MKOA WA PWANI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa pole kwa familia ya  Marehemu Mzee Rashid Kazinyingi  aliyekuwa Shekhe Mkuu wa kijiji cha Msata, wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani Jumatatu Agosti 6, 2012. Marehemu Mzee Kazinyingi, aliyefariki jana akiwa na umri wa miaka 88  pia alikuwa kada wa siku nyingi wa CCM.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishiriki katika kumuombea dua  Marehemu Mzee Rashid Kazinyingi aliyekuwa Shekhe Mkuu wa kijiji cha Msata, wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani Jumatatu Agosti 6, 2012. Marehemu Mzee Kazinyingi, aliyefariki jana  akiwa na umri wa miaka 88, pia alikuwa kada wa siku nyingi wa CCM.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kwenye kaburi la Marehemu Mzee Rashid Kazinyingi aliyekuwa Shekhe Mkuu wa kijiji cha Msata, wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani Jumatatu Agosti 6, 2012. Marehemu Mzee Kazinyingi, aliyefariki jana akiwa na umri wa miaka 88, pia alikuwa kada wa siku nyingi wa CCM.
(PICHA NA IKULU)

Saturday, February 4, 2012

MAKAMU WA RAIS DK GHARIB BILAL AKAGUA UJENZI WA SHIRIKA LA ELIMU KIBAHA, AZINDUA TAASISI YA UTAFITI WA MARADHI YA MALARIA, BAGAMOYO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (katikati)akikata utepe kuzindua Kituo cha Taasisi ya utafiti wa maradhi ya Malaria kilichopo Bagamoyo, wakati alipokuwa katika ziara yake ya Wilaya ya Bagamoyo, mkoa wa Pwani jana Februari 03, 2012. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muunganon wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea na kukagua ndani ya jengo la Shirika la Elimu Kibaha, wakati alipokuwa katika ziara yake ya Wialaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani leo Februari 04, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungno wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Dkt. Isaack Lwali (wa pili kulia) wakati alipotembelea na kukagua ujenzi wa Jengo la Shirika la Elimu Kibaha, wakati akiwa katika ziara yake ya Wilaya ya Kibaha mkoa wa Pwani leo Februari 04, 2012. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Elimu Kibaha, Dkt. Cyprian Mpemba.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungno wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Dkt. Isaack Lwali (wa pili kulia) wakati alipotembelea na kukagua ujenzi wa Jengo la Shirika la Elimu Kibaha, wakati akiwa katika ziara yake ya Wilaya ya Kibaha mkoa wa Pwani leo Februari 04, 2012. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Elimu Kibaha, Dkt. Cyprian Mpemba
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea na kukagua jengo la Shirika la Elimu Kibaha, wakati akimalizia ziara yake ya Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani leo Februari 04, 2012. Kushoto ni Dkt. Isaack Lwali (wa pili kushoto) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Elimu Kibaha, Dkt. Cyprian Mpemba. 
Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi ya Makamu Wa Rais