SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Sunday, June 15, 2014

MAMIA WAMZIMKA MAREHEMU BONDIA IRAQ HUDU 'MKUMWENA' KIMBUNGA KATIKA MAKABURI YA KISUTU


Jeneza lililokuwa na mwili wa marehemu Iraq Hudu 'Mkumwena' wakipeleka mwili kuzika katika makaburi ya Kisutu Dar es salaam kwa ajili ya kumuhifadhi 
 Mwili wa Iraq Hudu ukishushwa katika gari maalumu wakati wa mazishi yake katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam.
Baadhi wa waombolezaji wakiwa wamebeba jenza lililokuwa na mwili wa bondia wa zamani wa ngumi za kulipwa Iraq Hudu ‘Kimbunga’ wakati wa mazishi yake yaliyofanyika jana katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam. 
Mazishi ya bondia Iraq Hudu yakifanyika leo katika makaburi ya Kisutu.


Baadhi ya waombelezaji wakitia udongo katika kaburi la marehemu Iraq Hudu wakati wa maziko yaliyofanyika leo katika makaburi ya Kisutu Dar es salaam 
Baadhi ya waombelezaji na mabondia wakiwa nyumbani kwa marehemu Iraq Hudu kutoka kushoto ni bondia Adwer George, Rashidi Matumla, Rais wa Oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini Yasini Abdallah na Mwenyekiti wa Shiwata Cassim Twalibu 
Mtoto wa Marehemu Iraq Hudu, Daniel Hudu  kushoto akisalimiana mabondia Adrwe George,Rashidi Matumla na Rais wa TPBO Yassin Abdallah
Mtoto wa Marehemu Iraq Hudu, Daniel Hudu  kushoto akisalimiana mabondia Adrwe George,Rashidi Matumla na Rais wa TPBO Yassin Abdallah
Mashekhe wakisoma duwa kabla ya kwenda kuzika
Meneja wa bendi ya msondo ngoma Said Kibiriti akisalimiana na mabondia
Baadhi ya waombelezaji waliojitokeza
Mtangazaji Maulid Baraka Kitenge akizungumza na mabondia mbalimbali wakati wa msiba wa bondia Iraq Hudu
Mtangazaji wa kipindi cha Michezo Maulid Baraka Kitenge akisalimiana na bondia mkongwe ambaye kwa sasa ni kocha wa MKoa wa Tanga katika wilaya ya Muheza Chales Muhilu 'Spins'
Bondia Marehemu Iraq Hudu 'Kimbunga' kulia enzi za uhai wake katikati ni marehemu bondia Papa Upanga
Bondia Iraq Hudu' Kimbunga kulia akipambana na Stanley Mabesi katika mpambano wao
Marehemu IRAQ HUDU
WAOMBWELEZAJI WAKIWA WAMEBEBA JENEZA LA MAREHEMU IRAQ HUDU
WAOMBWELEZAJI WAKIWA WAMEBEBA JENEZA LA MAREHEMU IRAQ HUDU
Mmoja wa waombelezaji kulia akimpa pole bondia Chuku Duso katika msiba wa bondia Iraq Hudu
Ibrahimu Kamwe na Said Chaku
wadau mbalimbali wa mchezo wa ngumi
WAOMBWELEZAJI WAKIWA WAMEBEBA JENEZA LA MAREHEMU IRAQ HUDU


WAOMBELEZAJI WAKITIA UDONGO KWENYE KABURI LA MAREHEMU IRAQ HUDU
WAOMBELEZAJI WAKITIA UDONGO KATIKA KABURI LA IRAQ HUDU
WAOMBELEZAJI WAKITIA UDONGO KATIKA KABURI LA IRAQ HUDU 

PICHA NA Super Boxing Coach

Na Francis Dande

MAMIA ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake, wakiwemo wanamichezo, leo wamejitokeza katika mazishi ya bondia wa zamani wa masumbwi ya kulipwa, Iraq Hudu (49).

Hudu, maarufu kama ‘Kimbunga’, aliyefariki dunia Ijumaa mjini Dar es Salaam, amezikwa jana majira ya saa 10:00 alasiri katika makaburi ya Kisutu, jijini Dar es Salaam.

Bondia huyo aliyewahi kutamba vilivyo katika ulingo wa masumbwi, alifariki alfajiri ya Ijumaa katika hospitali ya Hindu Mandal, akisumbuliwa na tatizo la ini na figo kutofanya kazi.

Hudu alizaliwa mwaka 1965 Ujiji Kigoma, na kupata elimu ya msingi mkoani humo na baadae kuja Dar es Salaam ambako alipata elimu ya sekondari.

Baada ya hapo, alijiingiza katika masumbwi katika miaka ya 1990 hadi miaka ya 2000, alipoacha. Marehemu ameacha watoto watatu.