Mabadiliko katika serikali yalitarajiwa kufanyika ,lakini mwandishi wa BBC katika mji mkuu wa Mali Bamako,anasema kuwa kiwango cha mabadiliko hayo hakikutarajiwa.
Waziri mkuu mpya ,Moussa Mara amekuwa mpinzani mkuu wa rais Boubakr Keita hapo awali
Bwana Mara aliye na umri wa miaka 39 amekuwa akiitaka serikali kuimarisha usalama katika eneo la kazkazini la nchi hiyo.