Mtafiti
wa Magonjwa ya Binadamu kutoka Taasisi ya Utafiti ya Magonjwa ya
Binadamu Tanzania (NIMR), Dk. Kijakazi Mashoto akiasilisha utafiti wake
juu ya Ugonjwa wa Kipindupindu alioufanya Mkoa wa Pwani katika Wilaya ya
Kisarawe.
NIMR
wameingia katika siku ya pili ya mkutano wao wa 28 wa Mwaka pamoja na
Kongamano la Wanasayansi Watafiti linaloendelea jijini Dar es Salaam
katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam.
Mtafiti
Mwandamizi kutoka Maria Stop Tanzania, Mengi Ntinginya akizungumza mara
baada ya kuwasilisha tafiti yake ya utikanaji wa huduma za afya ya
uzazi kwa watu wenye ulemavu.
Mkurugenzi wa NMR, Dk. Mwele Malecela akichangia katika tafiti zilizowasilishwa.
Mtafiti
kutoka DUCE, Dk. Jared Bakuza akiwasilisha tafiti yake aliyoifanya juu
ya hali ya ugonjwa wa Kichocho cha tumbo kwa Wilaya ya Kigoma vijijini
ambapo utafiti ulibaini 80% ya waliofanyiwa utafiti ambao walikuwa
watu 470 walikutwa wana maambukizi ya ugonjwa huo mabapo pia 10% ya
Nyani 150 waliofanyiwa utafiti katika Msitu wa Gombe pia wamekutwa na
maambukizi ambayo kwa mujibu wa utafiti huo hakuna tofauti kati ya
vimelea vilivyokutwa kwa binadamu na nyani hao.
Mtafiti, Dk. Safari Kinung'h akiwasilisha utafiti wake.
Dk. Upendo Mwingira akiwasilisha ripoti ya utafiti wake wa magonjwa ya binadamu mbele ya watafiti wenzake hii leo.
Watafiti chipukizi nao waliendelea kuwasilisha taarifa za tafiti zao
Wanasayansi watafiti wakifuatilia kwa makini..
Watafiti wakitoa pongezi kwa tafiti nzuri zilizowasilishwa.